Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Watanzania Waaga Mwaka 2018, Wataja Mambo Saba Yaliyowagusa
Dec 31, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_39342" align="aligncenter" width="1000"] : Bibi. Daniella Massinga Mkazi wa jiji la Dodoma akizungumzia mambo makubwa yaliyofanywa na Serikali katika kipindi cha mwaka 2018 leo.[/caption]

Na. Jacquiline Mrisho - MAELEZO

Wakati dunia nzima ikisubiri kwa hamu kubwa ifike saa sita kamili za usiku ili kuuaga mwaka 2018 na kuukaribisha mwaka 2019, kwa upande wa Tanzania, wananchi wameeleza na kuoa maoni yao juu ya mambo mbalimbali yaliyotekelezwa na kuufanya mwaka 2018 kuwa ni wa kipekee.

Mosi: Katika mahojiano hayo maalumu, Mkazi wa Dodoma, Bi. Daniella Masenga, ameeleza kufurahishwa na hatua ya Rais Magufuli kumaliza utata wa suala la Kikokotoo cha mafao ya wastaafu kwa kuagiza vikokotoo vya zamani viendelee kutumika mpaka mwaka 2023.

"Kwa kweli Watanzania tunapaswa tumshukuru Rais wetu kwa sababu amejitolea kupigania haki za wanyonge kwa kufanya maamuzi mengi magumu ambayo sio rahisi kiongozi mwingine. Rais amewatetea wafanyakazi ambao wameitumikia nchi hii jkwa uadilifu mkubwa kwa kuhakikisha wanapata pensheni zao vizuri”, alieleza Mama Masenga.

Pili, kuwasaidia Wajasiliamali wadogo. Kwa upande wake, bw. Fredrick Mbala, mfanya bishara wa Makole, Dodoma amemshukuru Rais Magufuli kwa ubunifu katika kutatua kero za wajasiliamali kwa kuwatengenezea vitambulisho vya biashara ambavyo vinawarahisishia mazingira ya kufanya biashara.

"Tunamshukuru sana Rais wetu kwa kutupigania na kutuwekea mazingira mazuri ya kutuendeleza kiuchumi, kwa sasa tunakaa kwa uhuru bila kunyanyasika. Rais huyu ni wetu na tunamuahidi hatuwezi kumuacha," alieleza Mbala.

[caption id="attachment_39343" align="aligncenter" width="1000"] Mkazi wa jiji la Dodoma ambaye ni mjasiriamali mdogo Bw. Fredirick Mbala akielezea afuraha yake kufuatia Serikali kuwapatia Vitambulisho vya Wajasiriamali wagodo vinavyowawezesha kufanya shughuli zao bila kubugudhiwa wakati wa mahojiano na maalum kuhusu utekelezaji wa Serikali kwa kipindi cha mwaka 2018 leo.[/caption] [caption id="attachment_39344" align="aligncenter" width="1000"] Mkazi wa jiji la Dodoma ambaye ni mjasiriamali mdogo Said Ally akielezea furaha yake kufuatia Serikali kuwapatia Vitambulisho vya Wajasiriamali wagodo vinavyowawezesha kufanya shughuli zao bila kubugudhiwa wakati wa mahojiano na maalum kuhusu utekelezaji wa Serikali kwa kipindi cha mwaka 2018 leo.[/caption]

Tatu, Ujenzi wa Miundombinu: James Rigangira ambaye ni Mfanyabibiashara na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Kampuni za Ulinzi mkoani Arusha ameipongeza Serikali kwa kuimarisha miundombinu ikiwemo ujenzi wa Reli ya Kisasa ya “Sandard Gauge”, ujenzi wa barabara ya juu ya Tazara maarufu kama Daraja la Mfugale, upanuzi wa barabara ya Kimara jiji Dar es Salaam mpaka Kibaha mkoani Pwani pamoja na ujenzi wa daraja la baharini la Selander na kulifufua Shirika letu la ndege kwa kununua ndege mpya za kisasa ni miongoni mwa mambo makubwa ambayo Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli imeyatekeleza.

“Kuna wakati nimekuwa najiuliza hivi kasi hii ya ujenzi wa miundombinu na utekelezaji wa ahadi za Serikali kwa wananchi ingekuwepo tangu Serikali za nyuma basin chi hii ingukuwa mbali sana kimaendeleo”, anaeleza Bw. Rugangila.

Nne, Kutatua Mgogoro wa Kodi kwa wafanyabiashara. Kwa upande mwingine Bw. Rugangila anataja mafanikio mengine ya Serikali kwa mwaka 2018 ni hatua ya Rais kuielekeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kukaa na wafanyabiashara kujadili namna bora ya ulipaji kodi badala ya Mamlaka hiyo kufunga maduka ya wafanyabiashara wanaodaiwa kodi.

“Mfanyabiashara na TRA wanapoingia katika mgogoro wa kodi, utatuzi wake sio kumfungia biashara yake, Serikali itazidi kupoteza mapato kwa kuikosa kodi kutoka katika biashara ambayo imeifunga. Tunamshukuru Rais aliliona hilo na tumemsikia jana (Jumapili) Waziri wa Fedha na Mipango akielekeza TRA isifungie biashara hovyo isipokuwa wadaiwa sugu na kwa kibali maalumu cha Kamishna Mkuu wa TRA”, alieleza.

[caption id="attachment_39346" align="aligncenter" width="1000"] Wananchi wakijipatia huduma toka kwa wajasiriamali wadogo maarufu kama wamachinga katika eneo la Makole jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_39345" align="aligncenter" width="1000"] Moja ya Barabara zilizofanyiwa maboresho katika jiji la Dodoma katika kikpindi cha mwaka 2018 kama inavyoonekana katika picha. (Picha na: MAELEZO)[/caption]

Tano, Huduma za afya: Kwa upande wa huduma za afya, wananchi wameipongeza Serikali kwa kujenga vituo vya afya kuanzia ngazi ya Kata kwa kuweka vifaa vya kisasa. Pascus Machemba mkazi wa Dodoma, anasema kuwa hata watoa huduma za afya wamekuwa wakiwajali wagonjwa na kuwahudumia vizuri."Kwa mwaka ujao nategemea Rais wetu atatekeleza mambo mengi zaidi ya haya kwa sababu amepanga kuipeleka Tanzania katika nchi ya uchumi wa kati," alisema Machemba.

Sit, Elimu bure: Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu katika Shule ya Msingi Viwandani, jijini Dodoma, Thomas Nyoni, amemshkuru Rais Magufuli kwa kuboresha elimu hasa katika suala la utoaji wa elimu bure pamoja na kufanya marekebisho makubwa kwenye shule mbalimbali.

Pia amempongeza Rais Magufuli kwa kuongeza utoaji wa mikopo ambao unapelekea hata vijana ambao hawakuwa na matumaini ya kupata elimu ya juu kuweza kuipata elimu hiyo kupitia mikopo ya elimu ya juu. Serikali inatoa zaidi ya bilioni 23 kila mwezi kwa ajili ya kuhudumia elimu bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne na katika bajeti ya mwaka 2018/19, Serikali imeongeza bajeti ya mikopo ya elimu ya juu mpaka kufikia shilingi bilioni 427.5.

Saba, ununuzi wa korosho: Katika maeneo ambayo wakulima nchini hususani wa Korosho wataendelea kuukumbuka mwaka 2018 ni hatua ya Serikali kuamua kununua korosho za wakulima baada makampuni binafsi ya ununuzi wa zao hilo kutaka kununua kwa bei ya chini. “Sina la kusema zaidi ya kumpongeza Rais Magufuli kwa kuelekeza Serikali inunue korosho zetu kwani wafanyabiashara walikuwa wanataka tuuze kwa bai ya hasara”, anaeleza Mohamed Makwinya, mkulima wa korosho kutoka Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.

Pamoja na kuelezea kuridhishwa na utekelezaji wa Serikali kwa mwaka 2018, wananchi hao wamesema wanatarajia mwaka 2019 Serikali itaendelea kutekeleza ahadi zake ikiwemo kuimarisha miundombinu, maji, umeme vijijini, huduma za afya pamoja na kuendeleza kasi ya ujenzi wa Tanzania ya viwanda ambapo itaongza upatikanaji wa ajira pamoja na soko la bidhaa na mazao yanayozalishwa nchini.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi