[caption id="attachment_10660" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimuelezea Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson alipotembelea wodi ya watoto katika taasisi hiyo kwa ajili ya kutoa msaada. Dkt. Tulia kupitia Taasisi yake ya Tulia Trust kwa kushirikiana na Dstv, Twincity pamoja na TSN Supurmarket ametoa msaada wa jozi nne za TV na maziwa katoni mbili. Katikati ni Mkurugenzi wa Dstv Tanzania Maharage Chande.[/caption]
Na: Agness Moshi na Bushiri Matenda
Watanzania na wadau mbalimbali wa sekta ya Afya nchini wameombwa kuendelea kuisaidia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ili iendelee kufanya kazi kwa ufanisi na kutoa huduma bora.
Hayo yamesemwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Mfuko wa Tulia Trust Mhe.Tulia Akson, wakati akikabidhi msaada runinga nne na katoni mbili za maziwa vyenye thamani ya shilingi 1,000,000 vilivyotolewa kwa watoto waliopo kwenye Taasisi hiyo kwa ushirikiano na Dstv,TSN na Kampuni ya Twincity.
[caption id="attachment_10663" align="aligncenter" width="750"] Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiwa amembeba mmoja wa watoto waliolazwa katika Taaisisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alipotembelea wodi ya watoto hao kwa ajili ya kutoa msaada leo Jijini Dar es Salaam. Mhe. Dkt. Tulia kupitia Taasisi yake ya Tulia Trust ametoa msaada wa jozi nne za TV, maziwa ya unga pamoja na ving’amuzi vya Dstv.[/caption]Dkt.Tulia amesema msaada wa runinga unatimiza ahadi waliohaidi kwa taasisi hiyo na unamaana kubwa sana kwa sababu utawasaidia watoto wanaokaa hospitalini hapo kwa muda mrefu kujifunza ,na kuwaburudisha kwa kipindi chote cha matibabu ya awali kabla ya kufanyiwa upasuaji.
“Watoto hawa wanakaa muda mrefu hospitalini wakitibiwa hivyo wanashindwa kujumuika na wenzao kwa michezo jambo ambalo linawafanya wahisi upweke kwa kuwapatia runinga kutawasaidia kuondoa hali hiyo , kuwaburudisha na kuwapa nafasi ya kujifunza kupitia vipindi mbalimbali vinavyorushwa na king’amuzi cha DSTV”, alisema Dkt.Tulia
[caption id="attachment_10666" align="aligncenter" width="750"] Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akisalimiana na baadhi ya watoto wenye matatizo ya moyo waliolazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alipotembelea wodi ya watoto hao kwa ajili ya kutoa msaada leo Jijini Dar es Salaam. Dkt. Tulia kupitia Taasisi yake ya Tulia Trust kwa kushirikiana na Dstv, Twincity pamoja na TSN Supermarket ametoa msaada wa jozi nne za TV na maziwa katoni mbili.[/caption] [caption id="attachment_10678" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimueleza jambo Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson alipotembelea wodi ya watoto katika taasisi hiyo kwa ajili ya kutoa msaada. Dkt. Tulia kupitia Taasisi yake ya Tulia Trust kwa kushirikiana na Dstv, Twincity pamoja na TSN Supurmarket ametoa msaada wa jozi nne za TV na maziwa katoni mbili. Katikati ni Mkurugenzi wa DSTV Tanzania Maharage Chande.[/caption]Naye Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohammed Janabi amesema kuwa si watoto tu watakaofaidika kwani hata wazazi wao wataweza kujua mambo mbalimbali yanayoendelea Nchini kwa kuangalia taarifa za Habari zitakazokua zinaonyeshwa kupitia chaneli mbalimbali.
“ Sio watoto wote wanaokuja hapa wanatatizo la moyo peke yake wengine wanakuja wakiwa na Magonjwa mengine ambapo inabidi tuanze kuwatibia kwanza magonjwa hayo ambapo wakati mwingine yanachukua muda mrefu hivyo basi kwa kipindi chote hicho runinga hizi zitakua zikiwapa burudani, elimu kwa masomo mbalimbali kama vile kiingereza, hesabu kwa watoto wakubwa na kwa wale wadogo wataburudika kupitia katuni”,alisema Prof. Janabi.
Prof. Janabi ameongeza kuwa msaada wa maziwa waliopewa utasaidia kuimarisha afya za watoto wadogo wanaotibiwa kwani wapo wengine wamekuja wakiwa na Afya duni ,wengine wana magonjwa ya utapia mlo hivyo kupelekea kuchelewa kupatiwa matibabu.
Aidha,Prof.Janabi amemshukuru Dkt.Tulia kupitia Mfuko wake wa Tulia Trust kwa kuendelea kuhamasisha wadau mbalimbali kuipatia misaada Taasisi hiyo.
Kwa upande wake mtoto Mwamvita Hassani mwenye umri wa miaka 13 kutoka wilayani Kondoa kwa niaba ya watoto wanaotibiwa kwenye Taasisi hiyo ametoa shukrani zake kwa Naibu Spika na wadau waliowapa misaada hiyo.
[caption id="attachment_10670" align="aligncenter" width="750"] Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wenye matatizo ya moyo waliolazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alipotembelea katika taasisi hiyo kwa ajili ya kutoa msaada leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na: Idara ya Habari – MAELEZO.)[/caption]“Ninawashukuru sana kwakutuletea Tv na Maziwa,Tumefurahi na tunawaombea watuletee Tv zingine”, alisema Mwamvita.
Prof.Janabi amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia upatikanaji wa vitanda kwa ajili ya Taasisi hiyo kwani wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo swala la upungufu wa vitanda kwa wagonjwa kwani wanavitanda 128 tu ambavyo havikidhi mahitaji kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa wanaofika kwa ajili ya matibabu.