Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wakandarasi wa JNHPP Watakiwa Kuishi Katika Eneo la Mradi
Jan 13, 2020
Na Msemaji Mkuu

Na Zuena Msuya, Morogoro

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewataka wakandarasi na wahandisi wanaotekeleza ujenzi wa Mradi Bwawa la kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Bonde la Mto Rufiji wa Julius Nyerere (JNHPP) kuhamia na kuishi katika eneo la mradi kuanzia Januari 13,2020, baada ujenzi wa nyumba za wafanyakazi kukamilika.

Aidha aliwataka wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) pamoja na wale Wahandisi washauri wa mradi (TECU) kuhamia katika eneo la mradi kuanzia mwezi ujao baada ya nyumba zao kukamilika pia.

Dkt.Kalemani alitoa agizo hilo, Januari 12, 2020, alipofanya ziara ya kumi ya kukagua maendeleo na hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa mradi huo, tangu kusainiwa kwa mkataba na mkandarasi kuanza kufanya kazi wa mradi huo uliopo Rufiji.

Dkt. Kalemani alisema kuwa, kuanzia sasa hakuna sababu ya wafanyakazi wakandarasi wanaotekeleza mradi wa JNHPP, kuishi mbali na eneo la mradi kwa kuwa tayari ujenzi wa nyumba za wafanyakazi umekamilika.

“Hatupendi kuona wafanyakazi wa mkandarasi wanaishi Dar Es Salaam, wakati kazi inafanyika Rufiji, kuanzia kesho (Januari 13,2020) wakandarasi wote wahamie eneo la mradi, na wale wafanyakazi wa TANESCO na TECU wao watahamia kuanzia mwezi ujao baada ya nyumba zao kukamilika,” alisema Dkt.Kalemani.

Alisema tayari nyumba 8 zimekamilika zenye uwezo wa kubeba wafanyakazi 192, lengo la nyumba zinazojengwa ni kubeba zaidi ya wafanyakazi mia nne watakaokuwa wakiishi katika eneo la mradi.

Katika ziara hiyo pia, alimtaka mkandarasi wa mradi huo kuanza kupeleka mitambo tisa ya kufua umeme (Turbine) pamoja na vipuri vingine vinavyohitajika katika eneo la mradi kwa kuzingatia makubaliano ya mkataba, pia aliwataka TANESCO pamoja na TECU kuwa wazalendo katika kuhakiki ubora wa mitambo hiyo kwa manufaa ya Taifa na kuhakikisha inafika eneo la mradi kwa wakati uliopangwa.

Vilevile aliendelea kupiga marufuku wafanyakazi wageni kufanya kazi zinazoweza kufanywa na watanzania zikiwemo za vibarua, ulinzi, wauza vyakula na kadhalika na kwamba yeyote atakayekaidi maagizo hayo atachukuliwa hatua kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba.

“Tunataka kuona walinzi ni SUMAJKT au Jeshi la Wanyapori, sitegemei kuona mlinzi kutoka nje ya Tanzania akiwa pale getini,na endapo atakuwepo basi

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi