Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wakala wa Vipimo Waadhimisha Miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika, kwa Kufanya Ukaguzi wa Kustukiza
Dec 09, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_49690" align="aligncenter" width="750"] Afisa Vipimo kutoka Wakala wa Vipimo nchini, Bw.Mohammed akitoa maelezo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu matumizi ya kifaa cha kupimia vipimo vya kuuzia nyama, mara baada ya Kufanya ukaguzi wa Kustukiza katika mabucha ya Mwenge Jijini Dar es Salaam mapema leo Desemba 09, 2019[/caption]

Na. Mwandishi Wetu

Wakala wa Vipimo Nchini (WMA) imesema kuwa itaendelea kulinda maslahi ya watumiaji na afanyabiashara kupata stahiki sahihi katika manunuzi na uuzaji wa bidhaa zao kwa kutumia vipimo vinavyoendana na thamani ya pesa inayolipwa na mteja.

Akizunngumza Jijini Dar es Salaam katika ziara ya Kustukiza kwa Wafanyabiashara wa Mabucha, Kaimu Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Temeke, Krishna Mahamba amesema kuwa dhumuni la ziara hiyo ni kuangalia kama vipimo vinazingatiwa na wauzaji ili kuleta usawa kwa wateja na wauzaji hao.

“Katika kuadhimisha miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika, Wakala wa Vipimo leo tumeamu kufanya zoezi hili ambalo linafanyika Nchi nzima ili kulinda haki za biashara kwa wateja na wauzaji kwenye mabucha haya, kwani mara nyingi katika siku za sikukuu kama hizi wauzaji huwa wanachezea vipimo”, Krishna Mahamba Kaimu Meneje (WMA) Mkoa wa Temeke.

  [caption id="attachment_49691" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo Mkoa wa Temeke, Bw.Krishna Mahamba, akieleza jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa kutumia mizani iliyosawa kwa wauzaji wa mabucha , mara baada ya Kufanya ukaguzi wa Kustukiza katika mabuchani yaliyoko Mwenge Jijini Dar es Salaam mapema leo Desemba 09, 2019.[/caption]

Alieleza kuwa wafanyabiashara wa mabucha wanapaswa kutumia mizani iliyopimwa ili kumuwezesha mpata huduma katika mabucha yao kupata bidhaa kulingana na thamani ya pesa yake na kuweza kuleta usawa pande  zote mbili yaani mteja na muuzaji.

Naye Kaimu Meneje Wakala wa Vipimo Mkoa wa Kinondoni, Charles Mavunde alisema kuwa leo wakala wa vipimo imefanya zoezi hilo ili kuangalia kama wafanyabiashara wa Mabucha wanazingatia Sheria ya Vipimo nchini Sura namba 340 ambayo inamtaka mfanyabiashara kutumia vipimo sahihi kulingana na bei ya bidhaa yake aliyoipanga kwa wanunuzi.

Mavunde alito wito kwa watanzania kuwa wanapokuwa wanaadhimisha sikukuu kama ilivyokuwa leo miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika wawe makini na wafanyabiashara katika sehemu zote za biashara kuanzia kwenye mabucha, sokoni na kwenye vituo vya mafuta kwa kuwa siku hizo wafanyabiashara huchezea vipimo na kutoa bidhaa kwa kuwapunja wateja wao.

  [caption id="attachment_49692" align="aligncenter" width="750"] Mmoja ya Wauzaji wa mabucha yaliyoko Mwenge Jijini Dar es Salaam, Petro Makole, akieleza jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa kutumia mizani iliyosawa kwa wauzaji wa mabucha , mara baada ya Kufanyiwa ukaguzi wa Kustukiza buchani kwake Mwenge Jijini Dar es Salaam mapema leo Desemba 09, 2019.[/caption]

Kwa upande wake, Meneja Mawasiliano kutoka (WMA), Irene John alisema kuwa wakala wa vipimo hawajalala katika siku za sikukuu, wataendelea kufanya ziara za kustukiza kwenye sehemu mbalimbali za biashara ikiwemo kwenye mabucha, sokoni na Vituo vya mafuta ili kuleta usawa kati ya Muuzaji na Mteja kupata stahiki zao kulingana na thamani ya pesa inayolipwa.

“Katika Maadhimisho haya ya Miaka 58 Uhuru Tanganyika hatujalala tumefanya zoezi la kaguzi wa kustukiza kwenye mabucha hapa Mwenge Jijini Dar es Salaam na zoezi hili linafanyioka nchi nzima, na lengo kuu ni kulinda stahiki za wateja na wauzaji ili kila mtu akitoa pesa ya lita moja apate lita moja, akitoa pesa ya kilo moja vilevile apate kilo moja”, Irene John Meneja Mwasiliano (WMA).

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi