[caption id="attachment_38960" align="aligncenter" width="900"] Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 777 Mjini Singida baada ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge ( MKURABITA) kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha biashara zao na hivyo kutoa mchango katika ujenzi wa uchumi wa Taifa.[/caption]
Na: Mwandishi Wetu
Wajasiriamali 777 wa mjini Singida wamenufaika na mafunzo yaliyoandaliwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA) ili kuwajengea uwezo wa kurasimisha biashara zao na kutoa mchango stahiki katika ujenzi wa uchumi.
Akizungumza wakati akifunga mafunzo kwa wajsiriamali hao mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amesema kuwa Dhamira ya Serikali ni kuwawezesha wajasiriamali kufanya biashara kwa tija na kuchochea maendeleo.
[caption id="attachment_38961" align="aligncenter" width="787"] Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishaji kutoka Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge ( MKURABITA) Bw. Japhet Werema akizungumzia faida za mafunzo kwa wajasiriamali hao zaidi ya 777 waliopatiwa mafunzo ili waweze kurasimisha biashara zao.[/caption] [caption id="attachment_38962" align="aligncenter" width="900"] Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Bi. Severina Kilala akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 777 Mjini Singida baada ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge ( MKURABITA) kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha biashara zao na hivyo kutoa mchango katika ujenzi wa uchumi wa Taifa.[/caption]"Mafunzo haya yametolewa kwa namna itakayowawezesha wajasiriamali wetu hapa Singida kuwa na mfumo bora wa kufanya biashara na kuleta mabadiliko makubwa kwa wajasiriamali"
Akifafanua amesema kuwakila majasiriamali anapaswa kuwa mwadilifu, mzalendo na mwenye mpangilio mzuri wa namna yakuendesha biashara yake, anayethemini muda, anayetii sheria na kujali wateja anaowahudumia ili kuchochea ukuaji wa Biashara husika.
Aliongeza kuwa wananchi mkoani humo wana imani kubwa na Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwa inajali ustawi wa wanyonge ndio maana imeweka mkazo katika kuwawezesha kupitia mipango na pragramu mbalimbali zinazotekelezwa ikiwemo uwezeshaji kupitia MKURABITA unaolenga kuwapa ujuzi wa namna bora ya kufanya biashara.
[caption id="attachment_38963" align="aligncenter" width="900"] Mwanasheria wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA) Bi Jane Lyimo akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 777 Mjini Singida baada ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge ( MKURABITA) kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha biashara zao na hivyo kutoa mchango katika ujenzi wa uchumi wa Taifa.[/caption] [caption id="attachment_38964" align="aligncenter" width="850"] Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akimtunuku cheti Bw.Haji Ramadhani ambaye ni mjasiriamali wa mjini Singida wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 777 mjini humo baada ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge ( MKURABITA) kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha biashara zao na hivyo kutoa mchango katika ujenzi wa uchumi wa Taifa.[/caption]Aidha aliwaasa wajasiriamali hao kuhakiksiha kuwa wanatumia vizuri mikopo watakayopata kutoka katika taasisi za fedha ili iweze kuwasaidia kukuza biashara zao na kufikia malengo kusudiwa ya kuanzisha biashara husika.
Aliwaasa wajasiriamali hao kuelewa dhana ya kuchukua mkopo kuwa ni kukuza na kuendeleza biashara na sivinginevyo hivyo wajiepushe na tabia ya kukopa fedha na kuzielekeza katika masuala yasiyoendana naukuzaji wa biashara zao ili kuepeka migogogro na kurudisha nyuma juhudi za kukuza biashara hapa nchini.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishaji Bw. Japhet Werema amesema kuwa wajasiriamali hao wanayo fursa yakuendelea kujengewa uwezo kupitia kituo kimoja cha huduma kinachofunguliwa katika Manispaa ya Singida ili kuendeleza kazi yakuwahudumia wajasiriamali kwa karibu zaidi ambapo taasisi zote zinzohudumia wajasiriamali zitakuwa zikitoa huduma katika eneo moja na hivyo kupunguza usumbufu kwa wajasiriamali hao.
[caption id="attachment_38965" align="aligncenter" width="900"] Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya washiriki wa mafunzo mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 777 mjini Singida baada ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge ( MKURABITA) kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha biashara zao na hivyo kutoa mchango katika ujenzi wa uchumi wa Taifa.[/caption] [caption id="attachment_38966" align="aligncenter" width="900"] Afisa Matekelezo kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa wa Singida Bi. Ansifnda Rweyongeza akisisitiza jambo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishaji kutoka Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge ( MKURABITA) Bw. Japhet Werema mara baada ya hafla ya kufungwa kwa mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 777 mjini Singida baada ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge ( MKURABITA) kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha biashara zao na hivyo kutoa mchango katika ujenzi wa uchumi wa Taifa.[/caption] [caption id="attachment_38967" align="aligncenter" width="900"] Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishaji kutoka Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge ( MKURABITA) Bw. Japhet Werema akisisitiza jambo kwa mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi mara baada ya hafla ya kufunga kufunga mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 777 mjini Singida baada ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge ( MKURABITA) kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha biashara zao na hivyo kutoa mchango katika ujenzi wa uchumi wa Taifa. (Picha na MAELEZO, Singida)[/caption]Aliongeza kuwa dhamira ya mafunzo hayo ni kujenga uwezo kwa wajasiriamali hao ili warasimishe biashara zao na kuzingatia taratibu za uendeshaji biashara zenye tija kwa maslahi yao na Taifa kwa ujumla ambapo wamefundishwa kuhusu utunzaji wa kumbukumbu, umuhimu wa kodi, masuala ya hifadhi za jamii, Umuhimu wa urasimishaji biashara.
Naye Meya wa Manispaa hiyo Alhaji Gwae Chima amesema kuwa wanaipongeza MKURABITA kwa kuwajengea uwezo wajasirimali hao ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi.
Pia alipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa juhudi inazochukua katika kuwawezesha wananchi hasa wanayonge kote nchini ili washiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi.
Mafunzo kwa wajasiriamali hao zaidi ya 777 yamefanyika mjini Singida yakiratibiwa na kuendeshwa na MKURABITA kwa kushirikiana na Manispaa ya Singida.