Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wadau Wanaosimamia Kemikali Hatarishi Wakumbushwa Kujisajili
Oct 23, 2018
Na Msemaji Mkuu

  [caption id="attachment_37264" align="aligncenter" width="750"] Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, akiongea wakati wa ufunguzi wawarsha ya siku moja na wadau wanaojishughulisha na usimamizi wa mizigo ya kemikali hatarishi (Dangerous Cargo) nchini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, Da es Salaam leo.[/caption]

Na Jacquiline Mrisho 

Wadau wanaojihusisha na usimamizi wa kemikali hatarishi wamekumbushwa kutimiza matakwa ya Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali ya Viwandani na Majumbani Na. 3 ya mwaka 2003 inayowataka kujisajili na kuwa na kibali cha kufanya shughuli hizo.

[caption id="attachment_37262" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali, Bw. Daniel Ndiyo, akiongea wakati wa ufunguzi wa warsha na wadau wa kemikali juu ya usimamizi wa mizigo ya kemikali hatarishi nchini.[/caption]

Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Dkt. Fidelice Mafumiko ameyazungumza hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akifungua warsha ya siku moja iliyohusu usimamizi salama wa mizigo ya kemikali hatarishi kwa wadau wa kemikali iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania.

Dkt. Mafumiko amesema kuwa GCLA ilishaandaa mwongozo wa namna ambavyo kemikali hatarishi zinapaswa kusimamiwa ndani na nje ya bandari, mwongozo huo unabainisha matakwa ambayo wadau wote wanaotaka kujihusisha na kemikali hatarishi wanatakiwa kuyatimize na kuyafuata.

[caption id="attachment_37266" align="aligncenter" width="750"] Katibu wa Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania, Mhandisi Anthony Swai (kushoto),akiongea wakati wa warsha ya wadau wanaojishughulisha na mizigo ya kemikali hatarishi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Kulia ni Mkurugenzi wa kampuni ya PMM Estate (2001) Ltd, Dkt. Judith Mhina.[/caption]

"Nina taarifa kuwa, pamoja na uwepo wa matakwa ya kisheria juu ya usimamizi wa kemikali hatarishi bado kumekuwa na baadhi ya kampuni zinazojihusisha na usimamizi au utunzaji wa kemikali hizo bila kuwa na vibali hivyo nawakumbusha wadau kusajili kampuni zenu ili mfanye kazi katika mazingira yanayotakiwa", alisema Dkt. Mafumiko.

Amefafanua kuwa wadau wanaojihusisha na usimamizi wa mizigo ya kemikali ni wengi lakini hadi sasa kampuni moja ya PMM Estate (2001) Ltd ambayo inaendesha shughuli hizo ndiyo pekee imekamilisha taratibu za kuhifadhi kemikali hatarishi na kupewa kibali cha kufanya kazi hiyo.

[caption id="attachment_37268" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Ubora wa Bidhaa, Bw. Sabanitho Mtega, akiwasilisha mada kuhusu taratibu zinazopaswa kufuatwa kisheria ili kuweza kusimamia kemikali hatarishi nchini.[/caption] [caption id="attachment_37267" align="aligncenter" width="750"] Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyekaa katikati), Katibu Mkuu wa Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA), Mhandisi Anthony Swai (wa pili kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali, Bw. Daniel Ndiyo (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara, Bw. George Kasinga (kulia) na Mkurugenzi wa kampuni ya PMM, Dkt. Judith Mhina (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wengine wa warsha ya usimamizi wa mizigo ya kemikali hatarishi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam leo.[/caption]

Dkt. Mafumiko ametaja baadhi ya masuala ya msingi yanayohitajika katika usajili yakiwemo ya kuwa na hati ya madhara kwa mazingira yaani "EIA", Mpango wa Kujikinga, mtaalamu mwenye sifa zinazotambulika kwa ajili ya usimamizi pia kama mdau anatunza kemikali aina ya Sodium Cyanide, anatakiwa kuwa na eneo la kutosha ili aweze kutenganisha shughuli za kemikali hatarishi na shughuli za mizigo mingine, kujiandaa na kukabiliana na majanga pamoja na vifaa vya usalama kutegemea na aina ya kemikali hatarishi unayotaka kusimamia au kuhifadhi.

Ametoa rai kwa washiriki wa warsha hiyo kutimiza wajibu wao kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zinazohusiana na shughuli za kusimamia au kuhifadhi kemikali hatarishi pamoja na kuhakikisha wanatoa huduma bora bila kuathiri usimamizi au uhifadhi salama wa kemikali hizo kwani Tanzania ni nchi inayohudumia nchi nyingine kwa kusafirisha kemikali hatarishi kupitia bandari ya Dar es Salaam.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi