Na: Judith Muhina - MAELEZO, Mtwara
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amesema zoezi la awali la uhakiki wa Wakulima , maghala na Vyama vya Msingi vya Ushirika vilivyopokea korosho umekamilikana kuingiziwa fedha zao benki..
Waziri Asungwa amethibitisha hilo alipoongea na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara mapema jioni hii.
Waziri Hasunga amesema “Mpaka leo kuna jumla ya Vyama vya Msingi vya Ushirika 35 ambvyo vimekithi vigezo vya kulipwa. Hivyo zoezi linaloendelea katika National Microfinance Bank – NMB na kuingiza majina ya wakulima na wale wasio na account kufunguliwa na kuingize fedha kulingana na koroshoalizowasilisha ghalani.
Vyama hivyo vya Msingi kutoka Tandahimba Newala Cooperative Union 10 – TAMECU, Tunduru Agricultural Marketing Cooperative Union 6, TAMCU, Masasi, Mtwara na Nanyamba Cooperative Union – MAMCU 15, na Lindi - Mwambao Cooperative Union 4 ambayo inashirikisha Lindi Mji na Lindi Vijijini.
Aidha Waziri Hasunga amefafanua kuwa fedha hizo zimeingizwa NMB na Tanzania Agricultural Development Bank – TADB kama agizo lilivyosema . Pia, wakulima watambue kuwa korosho zote zilizopo ghalani ni za msimu huu na zina daraja la kwanza hivyo zinastahilini kulipwa kwa kiwango alichotamka Rais Magufuli.
Tanzania ina jumla ya viwanda 23 Tanzania nzima ambapo vikifanya kazi vyote kwa ufanisi vinauwezo wa kubangua korosho 120,000 na kuleta ajira kwa Watanzania takriban. Hata hivyo kutokana na ukosefu wa malighafi katika viwanda vya ndani na mitaji midogo ya wawekezaji wetu korosho inayobanguliwa kwa sasa ni elfu 29 tu. Ameongeza Waziri Hasunga.
Katika kuonyesha umuhimu wa zao la korosho kwa Watanzania Waziri Hasunga alisema kuwa jumla ya Kaya laki 750 zinalima zao la korosho na kuna jumla ya vyama vya Ushirika vya korosho 617, ambapo 503 vipo Mtwara lindi na Ruvuma, 98 vipo Mkoa wa Pwani na Tanga na 14.
Akionya tabia iliyojitokeza kwa baadhi ya wakulima wasio waaminifu Waziri Hasunga amesema kuwa wapo wakulima wanaoleta korosho chafu katika maghala ambazo zimeshapoteza ubora wake na zinaonekana ni za mwaka jana na kuwaomba waache mara moja .
Pia kuna wakulima wasio waaminifu wanaoleta korosho kutoka nchi ya jirani ya Msumbiji ambapo wameona Tanzania ina bei nzuri ya korosho na kuwaagiza waache mara moja kwa sababu sheria za kimataifa za biashara haziruhusu.
Alipoulizwa kuhusu hatua zilizochukuliwa kwa korosho magunia 152 yaliyokamatwa yakitokea Msumbiji Waziri alisema magunia yote yametaifishwa.Pia, akawaomba wakulima watoe ushirikiano katika kutoa taarifa zozote zenye lengo la kuharibu zoezi zima la ununuzi wa korosho.
Mwisho Waziri alitoa wito kwa wakulima kuwa waangalifu na fedha wanazoingiziwa wazichukue kwa mkupuo maana italeta madhara ya usalama wao na pia wajenge tabia ya kuweka akiba na kutumia kidogo kidogo wakikumbuka kuna madeni wanadaiwa na pia kuna msimu wa kilimo ujao unahitaji fedha kwa ajili ya kuzalisha korosho bora na nyingi zaidi kuliko mwak ahuu.
Katika kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya kuacha asilimia kadhaa ya korosho hapa nchini kwa ajili ya kuhamasisha ubanguaji na kuinua ajira kwa wananchi.