Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Vivutio vya Utalii vya Tanzania Kuanza Kuonekana Baidu Septemba Hii
Sep 01, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_46417" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania, Devota Mdachi (wa kwanza kulia) akikabidhi zawadi kwa mtaalam wa mtandao wa Baidu kutoka China katika Hafla ya kuwaaga wageni hao iliyofanyika Ofisi za Bodi ya Utalii Tanzania TTB Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_46418" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii (TTB), Jaji Thomas Mihayo akikabidhi zawadi ya kanga kwa mtaalam wa mtandao wa Baidu kutoka China katika Hafla ya kuwaaga wageni hao iliyofanyika Ofisi za Bodi ya Utalii Tanzania TTB Jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_46419" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii (TTB), Jaji Thomas Mihayo na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania, Devota Mdachi wakiwa katika picha ya pamoja na Wataalam wa mtandao wa Baidu kutoka China katika Hafla ya kuwaaga wageni hao iliyofanyika Ofisi za Bodi ya Utalii Tanzania TTB Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Na. Paschal Dotto-MAELEZO

Tanzania imeelekeza juhudi zake katika kuvutia watalii hasa wale kutoka nje ya nchi na ikilenga zaidi kuliteka soko la china lenye watu wengi duniani, ambapo kwa siku za karibuni Bodi ya utalii Tanzania ilifanya ziara kubwa ya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania katika Miji ya Beijing, Shanghao, Chengdu, Guangzhuo, Hong Kong, Najing na Changsha.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi wa Boti ya Utalii Tanzania (TTB) Jaji Thomas Mihayo, alisema kuwa matunda ya Ziara nchini China sasa yameanza kuonekana kwa kitendo cha kampuni ya Baidu kuja nchini kufanya mradi wa upigaji picha jongevu na mnato wa vivutio vya utalii Tanzania ili kuweza kuvitangaza katika mtandao huo wenye wafuasi zaidi ya milioni 700.

“Matunda ya ziara iliyofanyika katika Miji ya China yameanza kuonekana ambapo safari hii timu ya wataalam 11 kutoka katika kampuni kubwa za kimtandao nchini humo (Baidu) waliwasili nchini tarehe 22 Agosti ,2019 na kutembelea baadhi ya maeneno ya vivutio vya utalii hapa nchini kwa lengo la kupata picha jongevu na mnato ili kutangaza vivutio hivyo kwenye soko la utalii wa zaidi ya watu milioni 700 wanaoufuatilia mtandao huu wa Baidu”, Alisema Jaji Mihayo.

China ni moja ya nchi duniani ambao wanatumia mtandao wao wa baidu, kwa hiyo ni dhahiri kuwa utengenezaji wa makala na picha mbalimbali walizopata kutoka katika vivutio hapa nchini vitaweza kuongeza watalii kutoka China kwani picha hizo zitaonekana kwa watumiaji zaidi ya milioni 700 wa mtandao huo.

Aliongeza kuwa lengo la TTB ni kuiwezesha sekta ya utalii kupata watalii wengi kutoka China na kuongeza idadi ya watalii wa kigeni wanakuja kuitembelea Tanzania kutokana na kuona vivutio vitakawekwa kwenye mradi huo wa Wander Planet kutoka katika kampuni ya BAIDU, kuanzia Septemba 2019 na kuendelea.

Mihayo alisema kuwa kati ya nchi saba duniani Tanzania imeibuka kuwa nchi ya kwanza katika Mradi huo na ndiyo nchi pekee kutoka bara la Afrika na nchi zingine zinazolengwa na mradi huo ni kutoka mabara ya Amerika, Asia na Ulaya.

Wakiwa nchini wataalam hao wa mambo ya Picha jongevu na picha mnato walipata wasaa wa kutembelea maeneo mbalimbali ya utalii nchini ikiwemo Mji wa kihistoria Bagamoyo, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Makumbusho ya Oldvuai Gorge, Hifadhi ya Taifa Serengeti, ziwa Manyara, Mji wa Mwanza na Zanzibar. Na maeneo hayo yote yamechukuliwa picha ili kuweza kutangazwa katika mtandao huo mkubwa wenye wafuasi milioni 700 nchini China.

Aidha, Jaji Mihayo alisema kuwa lengo la ziara ya wataalam hao ni kupiga picha jongevu na mnato na kuandika taarifa za vivutio mbalimbali vya utalii katika maeneo waliyotembelea na kisha kuziweka kwenye mtandao wao, na wameahidi kutekeleza kama walivyolenga katika kutangaza utalii wa Tanzania nchini China ambapo baadhi ya taarifa za Shirika la Utalii Duniani(UNWTO) zinaeleza jinsi China ilivyo na soko kubwa la utalii Duniani.

“Takwimu za Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) zinaonesha kuwa China ni nchi ambayo ina soko kubwa la utalii duniani, mwaka 2018 wachina Milioni 130 walisafiri nje ya nchi huku Tanzania ikipokea watalii 32,773 idadi ambayo ni ndogo ukilinganisha na idadi ya watalii hao kutoka China kwenda nchi zingine, kwa hiyo juhudi hizi zinafanyika ili kuliteka soko la China kwenye sekta hii muhimu” Alisema Jaji Mihayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devota Mdachi alisema kuwa kampuni ya Baidu kutoka China imefanya vyema kuwaleta wataalam hao ili kutekeleza kazi ya kupiga picha jongevu na mnato na kuweza kutangaza utalii wa Tanzania nchini China kwenye soko la watu milioni 130 wanaotoka nje ya nchi kwenda kutalii sehemu mbalimbali Duniani.

“Tunaishukuru kampuni ya Baidu kutoka China kwa kuwaleta wageni hawa, kwani wameona na walichokiona kinatosha kabisa kwenda kukieleza nyumbani kwao China, Tanzania tuna vivutio vingi sana kwa hiyo picha na video zilizopigwa kwenye vivutio ambavyo kila mtu duniani anatamani kuviona na kuitembelea Tanzania zitasaidia kuleta watalii wengi kutoka China ”, alisema Mdachi.

Naye kiongozi wa msafaro huo Bibi Jin Xiaping, alisema kuwa kampuni ya Baidu imefanya kitu muhimu kwa kuwaleta wataalam hao, kwani wamekuja Tanzania ili kuona jinsi gani wataweza kutekeleza mradi huo(Wonder planet) kupiga picha jongevu na mnato na sasa wamefanya kazi yao, kwa hiyo kuanzia Septemba hii wataweza kuweka kwenye mtandao wao wa Baidu na kutangaza uzuri wa Tanzania kwenye soko la utalii China.

“Wataalam hawa 11 kila mmoja anazaidi ya wafuasi milioni mbili kwenye mitandao ya kijamii, kwa hiyo wamepiga picha jongevu, mnato na wataandika makala mbalimbali ili kuziweka kwenye mitandao yao na kuwezesha wafuasi wao kufahamu vivutio vya utalii vilivyoko Tanzania”,Alisema Xiaping

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi