Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Vijana Wapongeza Serikali Kuwajengea Uwezo Kilimo cha Vitalu Nyumba
Apr 08, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_41881" align="aligncenter" width="900"] Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Antony Mavunde akisisitiza jambo wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati wa ziara ya kamati hiyo kutembelea mradi wa ujenzi wa vitalu nyumba katika Wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma Aprili 06, 2019.[/caption]

Na Mwandishi Wetu

Wanufaika wa programu ya kukuza ujuzi eneo la kilimo cha kisasa kupitia teknolojia ya kitalu nyumba “green house” wameipongeza Serikali kwa kuendelea kuwawezesha katika masuala ya kilimo hicho na kujikwamua kiuchumi.

Pongezi hizo wamezitoa hii leo Aprili 06, 2019 wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ilipotembelea kukagua utekelezaji wa Programu ya ukuzaji ujuzi kwa vijana katika Wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma.

Katika kupongeza jitihada hizo wanufaika wa programu ya kilimo hicho walibainisha mafanikio ikiwemo, kupata ujuzi wa kilimo cha mazao mbalimbali, kujikwamua kiuchumi ikiwa ni sehemu ya kujipatia vipato halali pamoja na kusaidia upatikanaji wa ajira kwa vijana wanaowezeshwa elimu hiyo.

Mtaalam kutoka kampuni ya Holly green Bw. Octovian Lasway alieleza kuwa, zaidi ya vijana 100 wamenufaika na elimu ya kilimo cha kitalu nyumba katika Wilaya hiyo na kusaidia kuondokana na changamoto za ukosefu wa ajira nchini.

“Programu hii imekuja wakati sahihi na imesaidia kundi kubwa la vijana kwa kuzingatia mafanikio yatokanayo na kilimo hiki cha kisasa kinacholeta tija kwa kuwa na mazao bora na kuongeza kipato kwa wananchi,”alisisitiza Octovian.

[caption id="attachment_41882" align="aligncenter" width="800"] Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Manaibu Waziri kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanufaika wa mradi wa kukuza ujuzi mbele ya moja ya Kitalu Nyumba cha mfano katika Wilaya ya Chamwino kama kinavyoonekana ikiwa ni moja ya mikakati ya kuwainua vijana kupitia programu ya uwezeshaji inayotekelezwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.[/caption]

Akitoa maelezo kwa wanufaika hao, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde alieleza jitihada za Serikali katika kufikia kundi kubwa la vijana katika kuwawezesha na kuwajengea uwezo wa masuala ya ukuzaji ujuzi ili kuendelea kuongeza tija na kujikwamua kiuchumi kwa kuzingatia falsafa ya uchumi wa viwanda.

“Mradi umekusudiwa kutekelezwa kwenye Halmashauri zote 185 Tanzania Bara ambapo awamu ya kwanza itafikiwa mikoa 12 na Halmashauri 83 kwa lengo la kuwezesha vijana kuwa na ujuzi pamoja na stadi za maisha  ili kufikia malengo tuliyojiwekea kama Serikali,”alieleza Mavunde

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ajira wa ofisi hiyo Bw.Ally Msaki alieleza kuwa, mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati ya Serikali katika kutatua changamoto ya ajira kwa vijana na kuboresha kipato kwa watanzania.

[caption id="attachment_41890" align="aligncenter" width="900"] Mkurugenzi wa Ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Ally Msaki akiwa kwenye moja ya kitalu nyumba wakati wa ziara ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika Wilaya ya Dodoma mjini na Chamwino.[/caption]

“Mpango huu unalenga kufikia vijana 18800 nchi nzima ambapo kila Halmashauri itafikia vijana 100 na hadi sasa tumefikia halmashauri za mkoa 10, ikiwemo;Dodoma, Iringa, Mbeya, Ruvuma, Lindi, Mwanza, Simiyu, Geita, Shinyanga na Kagera,”alieleza Msaki

Naye Makamu mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Nagma Giga alifurahishwa na utendaji na bidii ya vijana hao na kuwaasa kuendelea kutumia  ujuzi huo kwa vijana wengine nchini.

Naye Naibu Waziri wa Ofisi hiyo anayeshughulikia Watu Wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa aliwataka vijana kutodharau kilimo kwa kuzingatia mchango wake katika kujikwamua kimaisha.

[caption id="attachment_41889" align="aligncenter" width="900"]  Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria wakitazama nyanya katika moja ya vitalu nyumba vilivyotembelewa na Kamati hiyo katika Wilaya ya Dodoma mjini.[/caption]

“Maisha hayapo kwenye karamu peke yake bali jembe linauwezo wa kuwatoa na kuwakwamua kiuchumi endapo kutakuwa na umakini na kujitoa kwa bidii,”alisisitiza Ikupa.

Kwa upande wake mwanagenzi Bw.Festo Ezikiel aliendelea kuipongeza serikali kuendelea kuwaamii na kuwajengea uwezo wa kilio cha kisasa cha kutumia kitalu nyumba.

“Tunaipongeza Serikali kutuamii na kutupa ujuzi kuhusu kilimo hiki nasi tunaahidi kushirikisha vijana wengine waliopo katika maeneo yetu ili kujikwamua kiuchumi,”alisema Ezekiel

[caption id="attachment_41888" align="aligncenter" width="800"] Sehemu ya miche ya nyanya katika kitalu nyumba kama inavyoonekana katika picha ikiwa tayari kumika katika kitalu nyumba.[/caption] [caption id="attachment_41884" align="aligncenter" width="900"] Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Holly Green Agric Mhandisi Octavian Lasway akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu namna walivyoweza kutekeleza Programu ya ujenzi wa vitalu nyumba katika halmashauri ya Wilaya ya Chamwino pamoja na kuwajengea uwezo vijana ili kufanya mpango huo unaotekelezwa na Ofisi ya Waziri mkuu.[/caption]   [caption id="attachment_41885" align="aligncenter" width="781"] Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Antony Mavunde akiwaongoza wajumbe  wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati wa ziara ya kamati hiyo kutembelea mradi wa ujenzi wa vitalu nyumba katika Wilaya ya Chamwino  na Dodoma Mjini Aprili 06, 2019.[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi