Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Ujerumani Wafungua Ofisi ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Nchini
Apr 18, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_30537" align="aligncenter" width="702"] Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Biashara na Viwanda (DIHK), Dkt. Martin Wansleben akizungumza katika tukio hilo wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi.[/caption]

Serikali ya Tanzania imesema kuwa itatumia vyema mahusiano yake baina ya nchi ya Ujerumani katika kuendeleza ukuaji wa uchumi kupitia viwanda na uwekezaji wa biashara nchini kwa kuimarisha maeneo ya kiuchumi ili wafanyabishara wa nchi hiyo waweze kuja kwa wingi katika uwekezaji.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage wakati wa ufunguzi rasmi wa Ofisi ya Kampuni ya AHK kutoka Ujerumani ambayo inawaunganisha wawekezaji na wafanyabishara wa Ujerumani ambao watakuwa na ofisi yao ya kudumu ili kuwa karibu na fursa za kiuwekezaji hapa nchini.

“Tunawakaribisha sana Wajerumani kupitia kampuni yao hii kubwa kabisa ya AHK. Tunaamini watatusaidia sana kutuletea wawekezaji wa Kijerumani hapa na watakuwa wanachukua bidhaa za Kitanzania na kupeleka Ujerumani.

[caption id="attachment_30538" align="aligncenter" width="702"] Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza katika ufunguzi huo.[/caption]

Sisi tunanunua vitu vingi kutoka Ujerumani. Kwa hiyo uwapo wao hapa nchini tutakuwa na maendeleo makubwa zaidi kwenye mahusiano yetu ya ukuaji wa uchumi kwa wao kununua vitu zaidi na kupeleka kwenye masoko ya Ujerumani” Alieleza Waziri Mwijage.

Kwa upande wao wakitoa ujumbe wa pamoja kwa Wanahabari, Dkt. Jennifer Schwarz na Balozi wa Ujerumani nchini, Dkt. Detlef Waechter, walibainisha kuwa, kwa sasa inaonesha kuongezeka kwa maslahi ya makampuni ya Ujerumani yanayokuja kufanya biashara na Tanzania hivyo kwa kuptia AHK, makampuni yataongezeka zaidi.

"Ujerumani na Tanzania wamekuwa marafiki wa karibu na washirika kwa muda mrefu. Soko la Tanzania linakuwa kwa kasi na kutoa fursa kubwa kwa biashara za Ujerumani. Makampuni kadhaa ya Kijerumani tayari yameanzisha viungo vya biashara na Tanzania, lakini tunataka kuvutia makampuni zaidi kutoka Ujerumani kwa kuwapa huduma wanazohitaji ili kuanza biashara yao Tanzania.

[caption id="attachment_30539" align="aligncenter" width="702"] Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa ofisi hiyo ya AHK kwa Tanzania.[/caption] [caption id="attachment_30540" align="aligncenter" width="702"] Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Biashara na Viwanda (DIHK), Dkt. Martin Wansleben mara baada ya kuzindua rasmi ofisi mpya ya AHK kwa Tanzania. (Picha zote na Mwandishishi Wetu).[/caption]

Makampuni ya Tanzania ambayo yanapenda kuanzisha viungo vya biashara kwa Ujerumani, pia yatasaidiwa. Hivyo AHK milango yake ipo wazi kwa wadau wote wa biashara katika kutoa njia za kufikia malengo ya ushirikiano huu” Walieleza.

Ofisi hiyo mpya iko eneo la Masaki barabara ya Chole na Slipway na itakuwa na ofisi zake mahali hapo. Kampuni hiyo ya AHK inafanya kazi kwenye nchi zaidi ya 90 Duniani kote na kwa Tanzania inakuwa ndio mara ya kwanza kufungua ofisi huku kwa Afrika Mashariki wakiwa na Ofisi nchini Kenya.

Aidha, Ofisi hiyo itaendeleza mahusiano ya biashara ya Ujerumani na Tanzania na kuwa kipaumbele kwa makampuni ya Ujerumani kutafuta fursa za biashara nchini huku ikitarajiwa kuongozwa na Dk Jennifer Schwarz na itatoa huduma mbalimbali kwa makampuni ya Tanzania na Kijerumani.

Wakati wa ufunguzi rasmi, wajumbe wa juu kutoka Ujerumani walitembelea Jiji la Dar es Salaam huku wakiongozwa na Dk. Martin Wansleben, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Biashara na Viwanda (DIHK).

Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa Biashara na Viwanda wakiwemo wafanyabishara, Mabalozi na wageni wengine wakiwemo kutoka Serikalini na Sekta binafsi.

 

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi