Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Makonda Kutafuta Bilioni 1 Kukopesha Waandishi wa Habari za Mitandaoni
Jan 13, 2026
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mhe. Paul Makonda akizungumza na Menejiment ya Wizara hiyo mara baada ya kuapishwa leo Januari 13, 2025 na
Na Baraka Messa – MAELEZO

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mhe. Paul Makonda, ameahidi kutafuta kiasi cha shilingi bilioni moja kwa ajili ya kuwakopesha waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii ili waweze kununua vifaa vya kisasa vya kazi na kuzalisha maudhui yenye kuitangaza Tanzania kimataifa.

Akizungumza Januari 13, 2026, katika ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma, wakati wa makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri Makonda alisema vijana wengi wamejiajiri kupitia majukwaa ya kidijitali na wanahitaji kuungwa mkono ili kuboresha kazi zao.

Amesema atamfikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ombi hilo kwa kuwa Mhe. Rais anaelewa na kuthamini mchango wa mitandao ya kijamii katika utoaji  wa habari na taswira ya nchi.

"Nitakwenda kumlilia  Dkt. Samia Suluhu Hassan ili atupatie shilingi bilioni moja tuwakopeshe vijana wanaofanya habari za mitandaoni wawe na kompyuta, kamera na vifaa vingine vya kurekodia ili waweze kutengeneza maudhui bora na yenye kuitangaza nchi yetu," amesema Makonda.

Aidha Mhe. Makonda, amewataka watendaji wote wa Wizara hiyo kuhakikisha wanafanya kazi kwa ufanisi na kuendana na kasi ya uongozi wake, ili kuijenga wizara kuwa na nguvu na mvuto kwa watumishi wa umma.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi