Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Samia Awapongeza Taifa stars kwa Kufika Hatua ya 16 Bora (AFCON)
Jan 10, 2026
Rais Samia Awapongeza Taifa stars kwa Kufika Hatua ya 16 Bora (AFCON)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanaume ya Tanzania ‘Taifa Stars’. Rais Mhe. Dkt. Samia aliwaandalia hafla ya chakula cha mchana na kuwapongeza wanamichezo waliofanya vizuri kimataifa, Ikulu jijini Dar es Salaam, tarehe 10 Januari 2026.
Na Timothy Mwakyenda - MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewapongeza wachezaji wa timu ya taifa ya Mpira wa miguu Tanzania, Taifa Stars kwa kufika hatua ya 16 bora ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mara ya kwanza tangu kuanza kushiriki mashindano hayo.

Rais Samia Ametoa pongezi hizo katika hafla ya kuwapongeza wanamichezo waliofanya vizuri katika ngazi ya kitaifa tarehe 10 Januari, 2026  katika ukumbi wa Ikulu Magogoni Jijini Dar es salaam. Fainali za mataifa ya Afrika kwa msimu wa 2025/2026 zimefanyika nchini Morocco ambapo Taifa Stars ilifanikiwa kufika hatua ya 16 bora.

Amesema kuwa katika mashindano ya AFCON kwa mwaka huu Taifa Stars imeleta mafanikio na heshima kubwa kwa taifa na ni ushahidi tosha wa kuionyesha dunia kuwa soka letu linakua na kupanda viwango vya juu barani Afrika.

"Hongereni sana, mmefanya kazi nzuri sana, na tunajua kwa nini yale yalitokea, kwa sababu tunajua wale ni wenyeji, ni taifa lenye fedha, ni taifa ambalo lina ushawishi kwa wenzetu hao waandaaji kwa sababu tulikuwa tunayaona wazi na Dunia imeyaona wazi kwamba Tanzania ina wapambanaji na wamepambana lakini lile ilibidi litokee iwe iwavyo lazima litokee hivyo, mimi nawapongeza sana". Amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia ameongeza kuwa, Tanzania inaelekea kuwa mwanyeji wa mashindano  ya AFCON 2027, hivyo maandalizi haya hayawezi kufanikiwa kama hakutokuwa na ushirikiano baina ya wadau mbalimbali wa michezo nchini

Amewataka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kushirikiana na wenzao wa TAMISEMI kuweka mipango mikakati mahiri ya kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya michezo kwa kuanzia ngazi za chini hasa mashuleni .

"Tunapokwenda AFCON muwe na mpango mahususi  wa kuchukua vipaji vya wale waliopo mashuleni, tuwanunulie tiketi waingie wakawaone wachezaji wa nje wanavyocheza ili watoto wetu wajifunze". Amesisitiza Rais Samia.

Sambamba na hayo amesema kuwa serikari itaendelea kujali maslahi ya wachezaji na kuziwezesha sekta binafsi kuwekeza katika michezo ili kuibua vipaji vipya vya ndani vitakavyotumika katika mashindano mbalimbali ya kimataifa

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi