Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Uchumi Wetu Haujawahi Kushuka kwa Miaka 10 Iliyopita – Dkt. Abbasi
Jun 15, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_51619" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi [/caption]

Na Jacquiline Mrisho

Serikali imesema kuwa uchumi wa Tanzania haujawahi kushuka kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita ikiwa ni malengo ya nchi iliyojiwekea kwa muda wa kati na mrefu kwamba uchumi wake ukue kwa zaidi ya asilimia 6.

Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amabaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wakati alipofanya majadiliano juu ya masuala mbalimbali ya kitaifa katika kipindi cha 360 kinachorushwa na Televisheni ya Clouds.

Dkt. Abbasi amesema kuwa Serikali imehamasisha watu kulipa kodi na inajitahidi kuhakikisha wananchi wanaiona thamani za kodi wanazozitoa. Amefafanua kuwa Serikali hiyo ilivyoingia madarakani makusanyo ya kodi kwa wastani yalikuwa Sh. bilioni 850 kwa mwezi lakini sasa Serikali inakusanya Sh. trilioni 1.5 kwa mwezi.

“Katika miaka mitano ya Serikali hii kazi kubwa imefanyika na sisi kama Serikali tumetimiza wajibu wetu, tunaiona nchi yetu inaendelea kupata maendeleo kwa kasi. Uchumi wetu haujawahi kushuka kwa miaka 10 iliyopita, kwa takwimu za Benki ya Dunia kama hali ya ukuaji wa uchumi ikiendelea hivi huenda mwaka 2021 au 2022 tukaingia kwenye uchumi wa kati lakini ule wa chini kidogo”, alisema Dkt. Abbasi.

Aidha, ameongeza kuwa nchi haiwezi kupata maendeleo ya watu bila kuwekeza kwenye vitu, ndiyo maana Awamu ya Tano imewekeza kwenye vitu ikiamini vitachagiza maendeleo ya watu kwani kila sekta ambayo Serikali imewekeza inachangia katika kuleta mageuzi kwa wananchi wa kawaida kwa kutoa ajira. Kwa takwimu zilizothibitishwa sekta ya viwanda pekee imeajiri watu zaidi ya 200,000.

Ameendelea kusema, Rais Dkt. John Pombe Magufuli anasisitiza dhana ya mabadiliko ya kifikra kwamba uchumi jumuishi utafikiwa sio tu kwa Serikali kuendelea kuwekeza katika miradi mbalimbali bali ni kwa Watanzania kuelewa na kutekeleza dhana ya kufanya kazi kwa bidii.

Akizungumzia kuhusu mradi wa bomba la mafuta, amesema kuwa mradi huo haujafa, ni wazo ambalo viongozi wamelipigania hivyo ni lazima litekelezeke. Kwa Tanzania hatua nyingi zimeshakamilika na kwenye mwezi Julai, 2020 Tenda zitaanza kutangazwa.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi