Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Ziara ya Rais Samia UAE Kufungua Milango ya Uwekezaji Tanzania
Feb 02, 2026
Ziara ya Rais Samia UAE Kufungua  Milango ya Uwekezaji Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kushiriki mkutano wa Dunia wa Serikali (World Governments Summit – WGS) 2026 pia atashiriki Jukwaa la Kimataifa wa Uwekezaji Afrika (GAIS).
Na Mwandishi Wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiondoka nchini kuelekea Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) leo tarehe 02 Februari, 2026, ambapo atashiriki kwenye mkutano wa World Government Summit (WGS 2026) na uzinduzi wa Global Africa Investment Summit (GAIS).

Ushiriki wa Tanzania katika WGS 2026 unaakisi utekelezaji wa DIRA 2050 na Sera Mpya ya Mambo ya Nje, zinazoweka diplomasia ya kiuchumi kama nguzo ya mahusiano ya kimataifa.

Lengo ni kuoanisha sera, ushirikiano na mitaji ya uwekezaji kwa maendeleo ya taifa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Al Maktoum (DWC) Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), tarehe 02 Februari, 2026.

Rais Mhe. Dkt. Samia atashiriki kwenye Mkutano wa Dunia wa Serikali (World Governments Summit – WGS) 2026pamoja na kushiriki Jukwaa la Kimataifa wa Uwekezaji Afrika (GAIS)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Waziri wa Sheria wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Abdullah bin Sultan bin Awad al Nuaimi mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Al Maktoum (DWC) Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), tarehe 2 Februari, 2026.

Rais Mhe. Dkt. Samia atashiriki kwenye Mkutano wa Dunia wa Serikali (World Governments Summit – WGS) 2026 pamoja na kushiriki Jukwaa la Kimataifa wa Uwekezaji Afrika (GAIS).

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi