Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano maalumu na Wakuu wa Taasisi za Utafiti katika Sekta ya
Kilimo pamoja Watendaji Wakuu wa Sekta Ndogo ya Mazao ya Kilimo uliofanyika ukumbi wa Mvuvi House Jijini Dar es salaam, Leo tarehe 11 Februari 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amesema ipo haja ya kuanzishwa kwa Sheria ya Kilimo itakayotoa suluhisho la changamoto zinazamkabili Mkulima na Sekta hiyo kwa
ujumla.
Waziri Hasunga ameyasema hayo leo tarehe 11 Februari 2019 wakati wa kikao cha siku mbili baina yake na Watafiti wa kilimo kutoka Taasisi mbalimbali
za kilimo nchini.
“Kuna kila sababu ya kuanzishwa haraka sheria ya kilimo, kwa sababu hatuna Sheria ya Kilimo na inayotumika sasa ni Sera ya
Kilimo, iliyotungwa mwaka 2013 ambayo pia inahitaji kupitiwa upya” amesema
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa akifuatilia kwa makini mkutano maalumu na Wakuu wa Taasisi za Utafiti katika Sekta ya Kilimo pamoja Watendaji Wakuu wa Sekta Ndogo ya Mazao ya Kilimo uliofanyika ukumbi wa Mvuvi House Jijini Dar es salaam, Leo tarehe 11 Februari 2019.
Mhe. Hasunga ameongeza kuwa Sheria zinazotumika kwa sasa ni za Bodi za Mazao mbalimbali, ambazo pia zinachangamoto
zake na kuna mazao ambayo hayana Bodi kiasi kwamba kuwatetea Wakulima wa mazao hayo inakuwa vigumu.
Mazao yaliyo katika utaratibu wa Bodi ni pamoja na zao la Pamba, Kahawa, Chai, Korosho, Pareto na Tumbaku kwa upande wa
mazao ya biashara, mazao ambayo hayana bodi ni yale ya chakula ambayo nayo yana mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa.
Waziri Hasunga amewataka Watafiti hao kutumia kikao hicho kutoa michango yenye tija, nini kifanyike katika Sekta ya Kilimo
kwakuwa Watafiti wana wigo mpana wa kuitoa Sekta hiyo kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akifuatilia kwa makini mkutano maalumu na Wakuu wa Taasisi za Utafiti katika Sekta ya Kilimo pamoja Watendaji Wakuu wa Sekta Ndogo ya Mazao ya Kilimo uliofanyika ukumbi wa Mvuvi House Jijini Dar es salaam, Leo tarehe 11 Februari 2019.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba alisema kikao hicho ni cha kipekee kwakuwa kimewakutanisha Wataifiti na
Wataalamu kutoka Taasisi za utafiti na watafiti wakufunzi wabobevu kutoka vyuo vya kilimo nchini.
“Ni furaha kuwaona leo hii kwa wingi wenu, eneo kubwa la kutiliwa mkazo ni katika suala la masoko, tunafanya tafiti nyingi
kuhusu mbegu bora lakini hatuna tafiti za kutosha kuhusu masoko ya mazao ya kilimo,” Alikaririwa Naibu waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa
Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo Naliendele Dkt. Fortunus Kapinga alisema kikao hicho kimekuja wakati muafaka
ambapo utafiti wenye tija na wenye kuzingatia wakati unahitajika zaidi ili kutatua changamoto za kilimo nchini.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akifuatilia mkutano maalumu na Wakuu wa Taasisi za Utafiti katika Sekta ya Kilimo pamoja Watendaji Wakuu wa Sekta Ndogo ya Mazao ya Kilimo uliofanyika ukumbi wa Mvuvi House Jijini Dar es salaam, Leo tarehe 11 Februari 2019.
Walioketi Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Katikati), Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Wa pili kutoka kushoto), Mhe Omary Mgumba (Wa pili kutoka kulia), Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe (Kulia), pamoja na Mshauri mwelekezi wa kilimo Prof Marcellina chijoriga wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Taasisi za Utafiti katika Sekta ya Kilimo pamoja Watendaji Wakuu wa Sekta Ndogo ya Mazao ya Kilimo uliofanyika ukumbi wa Mvuvi House Jijini Dar es salaam, Leo tarehe 11 Februari 2019.
“Kazi yetu Watafiti nikuhakikisha utafiti wa kina unafanyika ili kuondoa changamoto za wakulima, naamini tutabadilishana
uzoefu lakini pia tutaishauri serikali kuangazia katika tafiti zaidi na kutujengea uwezo ili tuzalishe tafiti zenye tija na uzalishaji bora,”alisema
Kikao kama hicho kitaendelea kesho Tarehe 12 Februari 2019 baina ya wizara na wadau wa kilimo wa sekta binafsi na baadaye kikao kama hicho
kitafanyika pamoja na wadau wa maendeleo ya kilimo wakimataifa na waliopo nchini.
Baada ya vikao hivyo Wizara na wadau wote wataamua muda gani sera ya kilimo ipitiwe upya na kuanzishwa mchakato wa muswada
wa sheria ya kilimo na hatimaye kupata sheria ya kilimo.