Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tumeweka Mbele Maslahi ya Wanachama Wetu - Mkurugenzi Mkuu NHIF
Feb 14, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_40477" align="aligncenter" width="800"] Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge (Katikati) akifuatilia utambulisho wa Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.[/caption]

Na: Grace Michael, Dodoma

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bw. Bernard Konga amesema kuwa mikakati yote inayowekwa na Mfuko huo inazingatia maslahi ya wanachama na wananchi kwa ujumla katika uimarishaji wa huduma za matibabu nchini.

Hayo ameyasema mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi la Mfuko ambalo limeketi leo kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yakiwemo ya uimarishaji wa huduma na mikakati ya kuwafikia wananchi katika maeneo yote.

[caption id="attachment_40482" align="aligncenter" width="600"] Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bw. Bernard Konga akitoa ufafanuzi wa jambo katika kikao hicho.[/caption] [caption id="attachment_40478" align="aligncenter" width="800"] Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa NHIF wakionyesha ishara ya Mshikamano wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi cha Baraza hilo ambacho kimeanza leo mkoani Dodoma.[/caption]

“Nikuhakikishie Mkuu wa Mkoa kuwa timu iliyoko hapa ya Wajumbe wa Baraza itahakikisha inaweka mipango inayozingatia maslahi ya wanachama wetu lakini pia utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuhakikisha kila mwananchi anakuwa kwenye utaratibu wa kupata matibabu kwa bima ya afya,” alisema Bw. Konga.

Alisema kuwa mikakati iliyopo kwa sasa ni kuyafikia makundi yote yakiwemo ya wakulima, wavuvi, wafugaji, wakwezi na makundi mengine na hili litafanikiwa kupitia uanzishwaji wa vifurushi vipya ambavyo vina gharama nafuu kwa kila mwananchi.

Mkurugenzi Mkuu alisema kuwa, Mfuko unatarajia kuzindua rasmi mpango wa vifurushi vipya mwezi Machi mwaka huu ambavyo vimeandaliwa kwa kuzingatia mahitaji halisi ya wananchi katika huduma za matibabu.

[caption id="attachment_40479" align="aligncenter" width="800"] Sehemu ya Wajumbe wa NHIF wakifuatilia hoja mbalimbali zilizowasilishwa katika kikao hicho.[/caption] [caption id="attachment_40480" align="aligncenter" width="800"]  Wajumbe wa kikao wakifuatilia agenda za kikao cha baraza.[/caption] [caption id="attachment_40481" align="aligncenter" width="800"] Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa NHIF walisimama kwa dakika moja kukumbuka watumishi ambao wamefariki katika kipindi kilichopita.[/caption]

Akifungua baraza hilo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Mahenge alisisitiza juu ya uwekaji wa mikakati ya kuwafikia wananchi wa ngazi zote ili kuwezesha kila mtanzania kuwa na uhakika wa kupata matibabu yenye wakati wowote anapopatwa na maradhi.

Alitumia fursa hiyo pia kuupongeza Mfuko kwa jitihada mbalimbali za uimarishaji wa huduma za matibabu nchini ikiwemo uwekezaji katika  ujenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa na maeneo mengine ambayo Mfuko umekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha miundombinu.

“Wajumbe wa kikao hiki hakikisheni mnatumia muda wenu vizuri kwa kuweka mikakati ambayo ni imara itakayoufanya Mfuko uhudumie watanzania wote lakini pia vizazi na vizazi,” alisema Mkuu wa Mkoa.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi