[caption id="attachment_27889" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akimwagilia maji mti aina ya Mkongo wakati wa programu ya kupanda miti Chuo Kikuu Dodoma[/caption] [caption id="attachment_27888" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akipanda mti wakati wa programu ya kupanda miti Chuo Kikuu Dodoma[/caption]
Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.
Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira imeendelea na kampeni yake ya Kijanisha Dodoma ambapo hii leo jumla ya miti 30,000 imepandwa katika Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) ikiwa ni utekelezaji wa kampeni hiyo mkoani humo.
akiongea wakati wa zoezi hilo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba amesema jawabu kubwa la kuondokana na ukame ni kupanda miti na kutokata miti.
"Dodoma ni miongoni mwa mikoa inayokabiliwa na jangwa, Serikali imeandaa mikakati mbalimbali pamoja na mkakati wa Taifa wa kupanda na kutunza miti wa mwaka 2016-2021 unaolenga kupunguza kasi ya uharibifu wa ardhi ili kuhakikisha kila mwananchi anahusika katika kupanda na kutunza miti," alisema Makamba.
[caption id="attachment_27887" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akaiongea mti wakati wa programu ya kupanda miti Chuo Kikuu Dodoma ambapo alizitaka Taasisi za Serikali kuacha matumizi ya Kuni na Mkaa na kuanza kutumia Gesi na nishati nyingine mbadala[/caption]Makamba amesema katika kudhibiti matumizi ya mkaa na kuni Serikali inatarajia kutoa muda usiopungua mwaka mmoja na nusu kwa Taasisi kubwa za Serikali kama vile Magereza, shule, vyuo na hospitali kuhama kutoka matumizi ya mkaa na kutumia gesi na nishati nyingine mbadala.
Hata hivyo amesema, matumizi ya mkaa yana gharama kubwa zaidi ukilinganisha na matumizi ya gesi, hivyo basi amewataka Watanzania kuacha matumizi ya mkaa na kutumia gesi na nishati nyingine ikiwa ni njia mojawapo ya kupunguza gharama wakati huohuo kutunza mazingira ya Mkoa naTaifa kwa ujumla.
Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Kangi Lugola amesema utunzaji wa mazingira sio suala la hiari ni la lazima, hivyo basi kila Mtanzania mahali alipo ana wajibu kupanda miti na si kusubiri mpaka Serikali kuleta kampeni za kupanda miti.
Nae, Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Antony Mavunde amesema Manispaa imepanga ratiba ya kupanda miti katika kila kata hivyo amewataka wananchi kuwa mstari wa mbele katika kupanda miti na kutunza mazingira.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amesema upandaji wa miti ni muhimu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwani athari zake ni kubwa na huitaji fedha nyingi kukabiliana nayo.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma (UDOM) Prof. Idris Kikula amesema chuo kimeamua kupanda miti 30,000 katika maeneo mbalimbali ya chuo pamoja na pembezoni mwa barabara katika kuadhimisha miaka 10 tangu chuo kilipoanzishwa mwaka 2007.
"Niishukuru Serikali kwa kutupatia miti, uongozi wa chuo umeweka mkakati madhubuti wa kuitunza miti hii hata baada ya mvua kuisha," alisema Prof. Kikula.
Kampeni ya Kijanisha Dodoma ilizinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Desemba 21, 2017 katika chanzo cha maji Bonde la Mzakwe.