[caption id="attachment_21095" align="aligncenter" width="1000"] Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro Bi. Siriel Mchembe akieleza mikakati iliyosaidia Wilaya hiyo kuongeza kiwango cha ufaulu hadi kufikia asilimia zaidi ya 70 mwaka huu kwa Shule za msingi wakati wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Walimu walipomtembelea Ofisini kwake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa Tume hiyo wanapotembelea Ofisi za watendaji wa Tume hiyo ngazi ya Wilaya.[/caption]
Frank Mvungi-MAELEZO- Gairo, Morogoro
Tume ya Utumishi wa Walimu imeanza kutekeleza kwa vitendo dhana ya Serikali ya Awamu ya Tano inayososisitiza uwajibikaji kwa kutoa mafunzo ya TEHAMA na utawala kwa Makatibu wasaidizi ngazi ya Wilaya ili kuongeza ufanisi na kukuza kiwango cha elimu nchini.
Akizungumza na Makatibu Wasaidizi wa Wilaya wakati wa kuhitimisha ziara ya Wajumbe wa Tume hiyo wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro, Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Devotha Gabriel amewasisitiza viongozi hao kuzingatia taaluma ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
“Mafunzo tunayowapa Makatibu Wasaidizi katika Wilaya zote yanalenga kuwajengea uwezo wa kutumia vifaa vya TEHAMA kwa kuzingatia sheria, kanuni pamoja na taratibu zote za Utumishi wa Umma ikizingatiwa eneo mojawapo tunalosisitiza ni kufuata taratibu za Utumishi wa Umma katika kuwahudumia walimu” Alisisitiza Devotha.
Bi. Devotha amesema kuwa utaratibu wa kuwajengea uwezo watumishi wa Tume hiyo ngazi ya Wilaya ni utekelezaji wa moja ya mikakati ya Tume hiyo ili kuongeza ufanisi katika kuwahudumia walimu ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
[caption id="attachment_21094" align="aligncenter" width="800"] Afisa Utumishi wa Tume ya Utumishi wa Walimu Bi. Anyagwe Lupembe akitoa ufafanuzi kuhusu taratibu sheria na Kanuni zinazotumika katika utumishi wa Umma kwa watumishi wa Tume ya utumishi wa Walimu Wilaya ya Gairo wakati wa ziara ya Ujumbe wa Tume hiyo.[/caption]Aidha Bi. Devotha alisistiza kuwa dhamira ya Tume hiyo ni kutekeleza maagizo yaliyotolewa hivi karibuni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Selemani Jafo katika kushughulikia masuala yote yanayowahusu walimu ndio maana Katibu wa Tume amekuwa akifuatilia na kuhakikisha maagizo hayo yanatekelezwa kikamilifu.
Utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Waziri unaenda Sambamba na kushughulikia masuala ya walimu kwa wakati na kujenga mifumo ya TEHAMA ambayo inawaunganisha Makatibu Wasaidizi katika ngazi ya Wilaya na Makao Makuu ya Tume hiyo hali itakayorahisha utendaji, kupunguza gharama,kuokoa muda na kutua changamoto za walimu kwa wakati.
[caption id="attachment_21093" align="aligncenter" width="800"] Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA wa Tume ya utumishi wa Walimu Bi. Devotha Gabriel akiwasiliosha mada kwa watumishi wa Tume hiyo Wilaya ya Gairo kuhusu matumizi salama ya vifaa vya TEHAMA pamoja na njia sahihi za mawasilisno kwa njia ya mtandao.[/caption]Aidha, Bi. Devotha alitoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza na kusaidia juhudi za Tume ya Utumishi wa Walimu katika kuimarisha utendaji kazi wa Tume hiyo kwa kujitolea vifaa vya TEHAMA na kuwajengea uwezo Makatibu Wasaidizi ngazi ya Wilaya.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Bi Siriel Mchembe amesema kuwa Wilaya hiyo imefanikiwa kukuza kiwango cha elimu hadi kufikia zaidi ya asilimia 70 ya ufaulu katika matokeo ya Darasa la saba.
[caption id="attachment_21097" align="aligncenter" width="1000"] Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro Bi. Siriel Mchembe (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe wa Tume ya utumishi wa Walimu uliongozwa na Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA wa Tume ya Utumishi wa Walimu Bi. Devotha Gabriel. Wa kwanza kulia ni Katibu Tawala wilaya ya Gairo Bw. Adam Bibangaba.[/caption]“Nimefanikiwa kusimamia kikamilifu ujenzi wa miundo mbinu kama madarasa, vyoo na miundo mbinu mingine hali ambayo imeongeza na kukuza morali ya walimu katika Wilaya yetu.” Alisisitiza Mchembe.
Akifafanua Mchembe amesema maendeleo ya sekta ya elimu katika Wilaya yake ni Kipaumbele na ameweka utaratibu mzuri wa kusimia utekelezaji wa mikakati ya kukuza elimu Wilayani humo.
Kwa upande wake Afisa Utumishi wa Tume hiyo Bi Anyagwe Lupembe amesema kuwa Tume hiyo imejikita kujenga uwezo kwa watumishi wake ili watimize majukumu yao kwa kuzingatia sheria Kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma.
Tume ya Utumishi wa Walimu imekuwa ikitekelza mpango wa kuwajengea uwezo Makatibu wasaidizi katika Wilaya zote nchini na kwa kuanza tayari mpango huo umetekelzwa katika mikoa ya Dodoma na Morogoro hivyo ni muda muafaka kwa wadau kujitokeza kuunga mkono juhudi hizo.