[caption id="attachment_21509" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maabara Hamishika 10 ilifanyika leo jijini Dar es Salaam. Maabara hizo zitakazotumiwa na TFDA katika kufanya ukaguzi wa ubora wa dawa nchini.[/caption]
Na. Paschal Dotto.
Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) imetakiwa kufuata ubora na ufanisi wa kazi yake ili kulinda maisha ya watanzania kwa kukagua dawa zilizo bora, salama na zenye ufanisi kwa matumizi ya afya ya binadamu.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa maabara hamashika (zinazohamishika) 10 za kupima ubora wa dawa.Uzinduzi uliofanyika Makao Makuu ya Mamlaka hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
[caption id="attachment_21510" align="aligncenter" width="750"] Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Matthieu Kamwa akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maabara Hamishika 10 zilizozinduliwa leo jijini Dar es Salaam. Maabara hizo zitakazotumiwa na TFDA katika kufanya ukaguzi wa ubora wa dawa nchini.Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Ushauri ya TFDA Bi. Zainab Thabit, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti Sillo na Kaimu Meneja wa Huduma za Maabara Dkt. Yonah Hebron.[/caption] [caption id="attachment_21511" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maabara Hamishika 10 zilizozinduliwa leo jijini Dar es Salaam. Maabara hizo zitatumiwa na TFDA katika kufanya ukaguzi wa ubora wa dawa nchini[/caption]Waziri Ummy alisema kuwa katika hali ya kuweka watanzania kwenye afya bora ni lazima Mamlaka hiyo izingatie ubora wa dawa na matumizi sahihi kwa binadamu na siyo kuachia uingizwaji wa dawa ambazo hazina ubora na usalama kwa afya ya binadamu.
“Mamlaka hii ni muhimu na iko sambamba na wananchi katika kuhakiki upatikanaji wa dawa, kwa hiyo mnatakiwa kudhibiti uingizwaji wa dawa ambazo hazina ubora, usalama na hazina ufanisi nchini maana zina madhara makubwa kwa wananchi”, alisema waziri Ummy.
Akibainisha utendaji kazi wa Mamlaka hiyo, Waziri Ummy alisema kuwa TFDA ni moja ya Mamlaka pekee inayofanya kazi nzuri katika Wizara ya afya na kuifanya Tanzania ijulikane kimataifa na Afrika kwa ujumla.
[caption id="attachment_21512" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maabara Hamishika 10 ilifanyika leo jijini Dar es Salaam. Maabara hizo zitatumiwa na TFDA katika kufanya ukaguzi wa ubora wa dawa nchini.[/caption] [caption id="attachment_21513" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa Maabara Hamishika wakifuatilia hafla hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Mbele kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Mkurugenzi wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu.[/caption]Aidha, Waziri Ummy alisema kuwa viwanda vya dawa ambavyo viko nchini vinatakiwa kuzingatia ubora wa kimataifa katika kuzalisha dawa kwa afya ya binadamu la sivyo Serikali haitanunua dawa hizo.
“hatutanunua dawa kwa wazalishaji wa ndani kama dawa hizo hazina vigezo hivi vitatu yaani ubora, usalama na ufanisi kwa ajili ya matumizi ya binadamu, TFDA endeleeni kufanya juhudi za kubainisha dawa zilizobora kwa kutumia teknolojia kama hii ya maabara hamishika ambazo zinarahisha kazi yenu”,alisisitiza Waziri Ummy.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw.Hiiti Sillo alisema kuwa katika kutambua uhitaji wa wananchi, Mamlaka hiyo itaendelea kuhakikisha kuwa maabara hizo zenye vifaa vya kisasa zinaendelea kutambulika kitaifa na kimataifa kwa kukidhi vigezo vya Shirika la Afya Duniani (WHO) na ISO/IEC 17025:2005 na mpaka sasa TFDA inashikilia vyeti vya ubora na umahiri ilivyovipata mwaka 2011 na 2012 kwa ufanisi katika kazi.
[caption id="attachment_21514" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Maabara Hamishika wakati wa hafla ya uzinduzi wa maabara hizo leo jijini Dar es Salaam. Maabara hizo zitatumiwa na TFDA katika kufanya ukaguzi wa ubora wa dawa nchini. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo, Mwakilishi wa Bodi ya Ushauri ya TFDA Bi. Zainab Thabit na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Matthieu Kamwa.[/caption] [caption id="attachment_21515" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Meneja wa Huduma za Maabara Dkt. Yonah Hebron akimwelezea Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wapili kushoto) namna Maabara Hamishika inavyofanyakazi mara baada ya kuzindua rasmi maabara hizo katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Maabara hizo zitatumiwa na TFDA katika kufanya ukaguzi wa ubora wa dawa nchini. Kutoka kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Matthieu Kamwa, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa TFDA Bi. Gaudencia Simwanza.[/caption] [caption id="attachment_21516" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wawakilishi wa taasisi zinazofanya kazi kwa kushirikiana na TFDA mara baada ya hafla ya uzinduzi wa Maabara Hamishika 10 iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Maabara hizo zitatumiwa na TFDA katika kufanya ukaguzi wa ubora wa dawa nchini. (Picha zote na: Frank Shija)[/caption]Aidha, alibainisha kuwa katika mpango huu wa maabara hamashika ulioanza mwaka 2002 walianza na maabara hamashika 10 katika vituo vya forodha (bandari ya Dar es Salaam) na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere pamoja na hospitali za Mikoa ya Mwanza, Arusha, Mbeya, Dodoma, Mara, Ruvuma na Kigoma kwa ufadhili wa Shirika la Afya Duniani (WHO) na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Management Science for Health (MSH) kutoka Marekani.
Aliongeza kuwa maabara hizo hamashika zilikamilika katika kipindi cha 2007/2009 hadi kipindi cha 2011/2013 na ziliweza kumudu uchunguzi wa sampuli 393 na awamu ya pili ilihusisha maabara zingine 5 katika mikoa ya Kagera, Iringa Rukwa na Manyara na kufanya kufika maabara 15 ambapo kiwango cha upimaji sampuli kiliongezeka kutoka sampuli 393 hadi sampuli 1485 mpaka sasa.
Sillo alisema kuwa katika jitihada za kufanya Afya ya wananchi iimarike, TFDA imeleta maabara zingine hamashika 10 na kujenga kituo kingine kikubwa Jijini Mwanza huku ikiajiri wafanyakazi 49 kati ya hao 27 ni wakaguzi na wachunguzi wa maabara 18 ili kuimarisha utendaji kazi katika mamlaka hiyo.