[caption id="attachment_39307" align="aligncenter" width="900"] Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (Mb) akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dodoma kuhusu hali ya uchumi wa Taifa na utekelezaji wa bajeti ya Serikali ambapo uchumi wa Tanzania umetajwa kuwa miongoni mwa nchi Tano bora kwa kasi ya ukuaji wa uchumi katika bara la Afrika katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka 2018.[/caption] Na; Mwandishi Wetu
Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa nchi Tano bora kwa kasi ya ukuaji wa uchumi katika bara la Afrika hali inayoonesha jinsi Serikali ya Awamu ya Tano ilivyojidhatiti kuwainua wananchi wake.
Akizungumza leo Jijini Dodoma kuhusu hali ya Uchumi wa Taifa na Utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa kipindi cha miezi 6 iliyopita, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (Mb) amesema kuwa nchi hizo ni Ethiopia asilimia (8.5) Ivory Coast (7.4) Rwanda (7.2) Tanzania(7.0) na Senegal (7.0).
Kwa upande wa Afrika Mashariki amesema kuwa uchumi wa Rwanda ulikuwa kwa asilimia (6.1) Uganda (5.1) Kenya (4.9) na Burundi (0.0) hali inayoonesha kuwa Tanzania bado imeendelea kuwa kinara kwa uchumi wake kukua kwa asilimia 7.1. [caption id="attachment_39308" align="aligncenter" width="900"] Sehemu ya washiriki wa mkutano wa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (Mb) na waandishi wa habari uliofanyika leo Jijini Dodoma wakifuatilia mkutano huo kuhusu hali ya uchumi wa Taifa na utekelezaji wa bajeti ya Serikali ambapo uchumi wa Tanzania umetajwa kuwa miongoni mwa nchi Tano bora kwa kasi ya ukuaji wa uchumi katika bara la Afrika katika kipindi cha nusu ya kwanza ya 2018.[/caption]“ Uchumi wa Taifa umeendelea kuwa imara, ukikua kwa wastani wa asilimia 7.1 (2017)ikilinganishwa na wastani wa ukuaji wa asilimia 7.0 kwa miaka miwili iliyopita kwa nchi za Afrika Mashariki na katika Afrika tumekuwa kati ya nchi Tano Bora Afrika”; Alisisitiza Dkt. Mpango
Akifafanua amesema kuwa kutokana na hali hiyo katika kipindi cha Januari hadi Juni 2018,Pato la Taifa lilikuwa kwa asilimia 7.0% ikilinganishwa na 6.3% katika kipindi kama hicho mwaka 2017.
Aidha alizitaja sekta zilizotoa mchango mkubwa katika pato la Taifa katika kipindi cha Januari hadi Juni 2018 kuwa ni Kilimo asilimia (34.5), Ujenzi (16.8) Biashara (10.1), Aidha sekta ya Kilimo ilikuwa kwa asilimia 3.6% kwa kipindi hicho.
“Thamani ya Shilingi ya Tanzania imeendelea kuwa tulivu, katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai hadi Novemba 2018,dola moja ya marekani ilibadilishwa kwa wastani wa Tsh 2,276 ikilinganishwa na Tsh 2,235 katika kipindi kama hicho mwaka 2017.” Alibainisha Dkt. Mpango.
[caption id="attachment_39306" align="aligncenter" width="900"] Watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (Mb) na waandishi wa habari uliofanyika leo Jijini Dodoma kuhusu hali ya uchumi wa Taifa na utekelezaji wa bajeti ya Serikali ambapo uchumi wa Tanzania umetajwa kuwa miongoni mwa nchi Tano bora kwa kasi ya ukuaji wa uchumi katika bara la Afrika katika kipindi cha nusu ya kwanza ya 2018.[/caption]Kwa upande wa sekta ya Benki pia imeendelea hadi kufikia Septemba 2018 kulikuwa na jumla ya benki na Taasisi za fedha zinazosimamiwa na Benki Kuu zipatazo 61 ambapo uwiano wa mitaji ya mabenki ikilinganishwa na rasilimali zao ulikuwa asilimia 16.3%, ikiwa juu ya kiwango kinachohitajika kisheria cha asilimia 10.0%.
Akizungumzia ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha miezi ya kwanza ya mwaka 2018/19 (Julai- Novemba) makusanyo ya ndani ikijumuisha mapato ya Halmashauri yalifikia shilingi Trilioni 7.37 sawa na asilimia 88.9 ya makadirio ya Shilingi Trilioni 8.30 katika kipindi hicho.
Aidha, kuhusiana na mfumuko wa Bei Dkt. Mpango amesema kuwa umeendelea kupungua kutoka wastani wa asilimia 4.3 kwa mwaka 2017/18 hadi kufikia kiwango cha chini kabisa kuwahi kutokea katika miaka ya karibuni cha asilimia 3.0 mwezi Novemba 2018.
Kwa upande wa fedha za kigeni akiba imeendelea kuwa ya kuridhisha na kutosheleza mahitaji ya kuiwezesha Tanzania kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje na pia kujenga imani ya wawekezaji. Akiba ya fedha za kigeni ilifikia dola za Marekani milioni 5,079.0 mwezi Novemba 2018, kiasi ambacho kinatosheleza kugharimia uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa kipindi cha takribani miezi 5.
Kuhusu Deni la Taifa Dkt Mpango amebainisha kuwa kwa Tathmini iliyofanyika mwezi Desemba 2018 inaonesha kuwa deni hilo ni himilivu kwa muda mfupi, wa kati na mrefu.Matokeo haya yanafanana na tathmini iliyofanywa na Shirika la Fedha Duniani (IMF).
Uchumi wa Tanzania unatarajiwa kuendelea kukua kutokana na uwekezaji mkubwa unaoendelea kwenye miundombinu wezeshi ya uzalishaji mali kama vile barabara, madaraja, bomba la mafuta, ujenzi wa reli kwa kiwango cha kimataifa na viwanja vya ndege, Ujenzi wa kituo cha kufua umeme wa maji katika mto Rufiji chenye uwezo wa kuzalisha MW 2100 kwa ajili ya matumizi ya majumbani na viwandani.