Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Taarifa kwa Umma - UTEUZI
Feb 14, 2019
Na Msemaji Mkuu

Ikulu, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Lucas Luhende Kija kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Taifa kwa Watu Wenye Ulemavu.

Dkt. Kija ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE).

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Michael Pius Nyagoga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Dkt. Nyagoga ni Kaimu Kamishna Msaidizi wa Sera, Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha na Mipango.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa wenyeviti hao umeanza tarehe 13 Februari, 2019.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

14 Februari, 2019

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi