Ikulu, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Richard Faustine Sambaiga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Sambaiga umeanza tarehe 23 Machi, 2019.
Dkt. Sambaiga ni Mhadhiri Mwandamizi, Idara ya Sosholojia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bi. Rukia Masasi ambaye amemaliza muda wake.
Wakati huohuo, Mhe. Rais Magufuli kesho tarehe 28 Machi, 2019 atamuapisha Mhe.Balozi Mteule Valentino Mlowola kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba.
Mhe. Balozi Mteule Mlowola ataapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 3:30 asubuhi.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
27 Machi, 2019