Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), TAHA- Taasisi inayosimamia Wadau wa Mbogamboga na Matunda kwa kushirikiana na Shirika la Biashara la Kimataifa (ITC) inatekeleza mradi wenye lengo la kuboresha masoko ili kuongeza mauzo ya Nje (MARKUP).
Hivyo, tunapenda kuwaataarifu wadau wa zao la parachichi nchini kushiriki katika mradi huo ili kufaidika na fursa ya upatikanaji wa mitaji ya biashara, mafunzo ya namna ya kufikia soko la nje,kuwa sehemu ya ushiriki wa Maonesho mbalimbali yatakayoenda sambamba na Mikutano ya kibiashara (B2B). KAMPUNI ZITAKAZOFAIDIKA NI ZILE TU ZITAKAZOKIDHI VIGEZO.
Ili kujisajili tafadhali tembelea tovuti www.tantrade.go.tz ili kujaza dodoso.Kwa taarifa zaidi piga simu Na. 0787 654386.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 14 Februari, 2019.
Imetolewa:
Theresa H. Chilambo
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
12 Februari, 2019