Ikulu, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Humphrey P.B. Moshi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ushindani nchini (The Fair Competition Commission - FCC).
Prof. Moshi ni Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Uteuzi wa Prof. Moshi unaanza leo tarehe 30 Oktoba, 2018.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
30 Oktoba, 2018.