Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Shindano la Kaizen Liwe Chachu ya Maendelo ya Uchumi wa Viwanda
Feb 18, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_51008" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof.Riziki Shemdoe akizungumza na washiriki wa programu ya KAIZEN katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi wa program hiyo ambayo inahusisha viwanda vidogo na vikubwa iliyofanyika katika Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Februari 18, 2020.[/caption] [caption id="attachment_51009" align="aligncenter" width="750"] Balozi wa Japan Nchini Tanzania, Mhe. Shinichi Goto, akizungumza na washiriki wa programu ya KAIZEN katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi wa programu hiyo ambayo inahusisha viwanda vidogo na vikubwa iliyofanyika katika Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Februari 18, 2020.[/caption]

Na Eric Msuya

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe amewataka washindi wa shindano la nne la KAIZEN lilopo chini ya usimamizi wa wizara ya Viwanda na Biashara, wakishirikiana na Shirika la Maendeleo kutoka Japani (JICA), kwenda kuitangaza vema Tanzania katika shindano kubwa la KAIZEN litakalofanyika mwezi septemba mwaka huu.

Akizungumza katika halfa ya kukabidhi tuzo  kwa washindi wa shindano hilo lilofanyika leo jijini Dar es Salaam, Prof. Shemdoe amesema kuwepo kwa shindano hilo ni  chachu kwa washindi katika kuitangaza Tanzania katika mashindano ya kimataifa ili kufikia lengo la uchumi wa viwanda 2025.

[caption id="attachment_51010" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw.Leo Lyayuka akitoa neno la shukurani kwa washiriki wa programu ya KAIZEN katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi wa program hiyo ambayo inahusisha viwanda vidogo na vikubwa iliyofanyika katika Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Februari 18, 2020.[/caption] [caption id="attachment_51011" align="aligncenter" width="750"] Wawakilishi kutoka kiwanda cha Shelly’s Pharmaceutical Tanzania, wakipokea tuzo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof.Riziki Shemdoe, baada ya kutangazwa washindi wa kwanza katika programu ya KAIZEN kundi la viwanda vikubwa katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi wa programu hiyo iliyofanyika katika Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Februari 18, 2020.[/caption]

“Niwapongeze sana washindi wa shindano hili la nne la KAIZEN katika falsafa ya kuongeza ubora na ubunifu, tuzo mtakazo pewa mzitumie katika kulitangaza vema taifa letu kwenye  shindano kubwa la KAIZEN barani Afrika litakalo fanyika mwezi septemba nchini Afrika ya Kusini” alisema Prof. Shemdoe

Aidha katika hafla hiyo amelipongeza Shirika la Maendeleo la Japan la (JICA) katika kuitekeleza sera ya Mhe. Rais magufuli “Tanzania ya Viwanda” ili  kufikia uchumi wa kati kwa ubunifu katika mashindano haya ya KAIZEN

[caption id="attachment_51012" align="aligncenter" width="750"] Wawakilishi kutoka kiwanda cha Kioo Limited wakipokea tuzo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof.Riziki Shemdoe, baada ya kutangazwa washindi wa pili katika programu ya KAIZEN kundi viwanda vikubwa katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi wa programu hiyo iliyofanyika katika Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Februari 18, 2020.[/caption] [caption id="attachment_51013" align="aligncenter" width="750"] Mwakilishi kutoka kiwanda cha Superdoll Limited akipokea tuzo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof.Riziki Shemdoe, baada ya kutangazwa washindi wa tatu katika programu ya KAIZEN kundi la viwanda vikubwa katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi wa programu hiyo ambayo inahusisha viwanda vidogo na vikubwa iliyofanyika katika Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Februari 18, 2020.[/caption]

“Niwapongeza sana JICA kwa Mkakati huu mzuri wa kutoa fursa kwa wadau kubadilishana uzoefu na kuhamasishana uendelevu wa tija ili kukuza sekta ya viwanda hapa nchini” alisema Prof.Shemdoe

[caption id="attachment_51014" align="aligncenter" width="750"] Mkufunzi wa Programu ya KAIZEN kutoka Chuo cha Biashara (CBE), Mariam Jambwe akipokea tuzo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof.Riziki Shemdoe, katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi wa program hiyo ambayo inahusisha viwanda vidogo vidogo na vikubwa iliyofanyika katika Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Februari 18, 2020.[/caption] [caption id="attachment_51015" align="aligncenter" width="750"] Mwakilishi kutoka kiwanda cha Tanzania Brush Product akipokea tuzo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof.Riziki Shemdoe, baada ya kutangazwa washindi wa kwanza katika programu ya KAIZEN kundi la viwanda vidogokatika hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi wa programu hiyo ambayo inahusisha viwanda vidogo na vikubwa iliyofanyika katika Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Februari 18, 2020.[/caption] [caption id="attachment_51016" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof.Riziki Shemdoe, akiwa kwenye picha ya pamoja na watendaji wa Wizara ya Viwanda na Biashara na KAIZEN mara baada ya kukabidhi tuzo kwa washindi wa Programu hiyo katika hafla iliyofanyika katika Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Februari 18, 2020.[/caption] [caption id="attachment_51017" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof.Riziki Shemdoe, akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa tuzo za KAIZEN mara baada ya kukabidhi tuzo hizo katika hafla iliyofanyika Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Februari 18, 2020.[/caption]

Naye Mkurugenzi wa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na   Biashara Bw. Leo Lyayuka ametoa rai kwa wadau wote wa sekta ya viwanda na biashara, kujiandaa vema na ubunifu wa hali ya juu na  kujituma katika kongamano la KAIZEN kwa  Nchi za Bara la Afrika 2021 litakaloanyika hapa Nchini.

“Tanzania tutakuwa wenyeji wa kongamano la KAIZEN katika bara la Afrika mwaka 2021, naomba kutoa rai kwa wadau wote  kujiandaa vema kushiriki na kupokea  ugeni huu, kujituma kwa dhati  na bila kusahau kutumia fursa hizo” alisema Lyayuka

Naye balozi wa Japani hapa Nchini Mhe. Shinichi Goto ameipongeza Serikali ya Tanzania katika sekta ya Biashara kwa kuendelea kuboresha mpango wa Utekelezaji wa kuboresha mfumo udhibiti wa Biashara Nchini (BluePrint)

“Niwapongeze sana kwa kuendelea kuboresha mfumo wa Blueprint, hii ni ishara ya kufikia malengo ya uchumi wa kati wenye viwanda nchini, mfumo huu ni muhimu na ni salama zaidi” alisema Balozi  Goto.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi