Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yavikumbusha Vyombo vya Habari Wajibu Wake Kwa Wananchi Kuelekea Mkutano wa SADC
Jul 13, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_45254" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi akizungumza wakati akifunga mafunzo kwa waandishi wa habari leo Julai 13, mjini Morogoro yakissslenga kuwajengea uwezo waandishi hao ili waweze kuandika na kuripoti habari za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusinini mwa Afrika (SADC), Mafunzo hayo yamefanyika kwa wiki moja yakihusisha awamu mbili za waandishi hao.[/caption]

Na Mwandishi Wetu- Morogoro

Serikali  imeviasa vyombo vya habari nchini kushiriki kikamilifu katika kutangaza   mkutano wa  wakuu wa nchi  na Serikali wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) hasa fursa zitakazowanufaisha wananchi.

Akizungumza wakati akifunga  mafunzo kwa waandishi wa habari takribani 60 yaliyofanyika mjini Morogoro kuanzia Julai 8 hadi 13, 2019  ili waweze kuandika na kuripoti kuhusu Jumuiya hiyo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji mkuu wa Serikali  Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa  jukumu la kujenga uelewa kuhusu fursa za mkutano huo ni la  waandishi wote kupitia vyombo vyao vya habari .

‘’Mnapotekeleza  wajibu wa kuandika na kuripoti habari za SADC mnapaswa kutoa maoni ya namna ya kuboresha ushiriki wetu katika Jumuiya za Kikanda  na kuonesha wapi tunapaswa kuboresha ili nchi yetu ifaidike zaidi na hata iwe mwenyeji bora wa mkutano huu” Alisisitiza Dkt Abbasi

[caption id="attachment_45255" align="aligncenter" width="592"] Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akieleza faida walizopata waandishi wa habari walioshiriki mafunzo kwa waandishi wa habari leo Julai 13, mjini Morogoro ikiwa ni awamu ya tatu ya mafunzo hayo yanayolenga kuwajengea uwezo waandishi hao ili waweze kuandika na kuripoti habari za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusinini mwa Afrika (SADC), Mafunzo hayo yamefanyika kwa wiki moja yakihusisha awamu mbili za waandishi hao.[/caption]

Akifafanua amesema kuwa vyombo vya habari vinapaswa kuitazama jamii  kwa ujumla na si Serikali peke yake kuepuka kuacha ule wajibu wa msingi wa vyombo hivyo  wa kuchangia kuleta ustawi wa wananchi na kutangaza utatuzi wa changamoto zinazoibuliwa  katika jamii.

 “Vyombo vya habari  vina wajibu wa kuwezesha wananchi  wa kawaida kupata taarifa sahihi na kwa wakati zikilenga kuwawezesha kujiletea maendeleo na hasa katika kipindi hiki ili waweze kutumia fursa za mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali za nchi wanachama wa SADC”.

Katika kutekeleza jukumu la kushirikiana na Serikali Dkt Abbasi amesema kuwa vyombo vya habari havipaswi kujikita katika kukosoa peke yake bali kusaidia katika vita ya kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa kuweka mbele maslahi ya nchi kwa kutumia kalamu na Kamera kwa ustawi wa wananchi.

Aliongeza kuwa mkutano wa SADC una fursa nyingi kwa wananchi ikiwemo katika usafirishaji na uchukuzi, malazi , utalii na nyingine nyingi hivyo jukumu la vyombo hivyo ni kuwajengea uwezo wananchi kuzitambua na kuzitumia ili waweze kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wao , Taifa na Jumuiya nzima ya SADC.

[caption id="attachment_45258" align="aligncenter" width="900"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwa kwenye picha ya pamoja na wawezeshaji wa mafunzo yanayolenga kuwajengea uwezo waandishi hao ili waweze kuandika na kuripoti habari za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusinini mwa Afrika (SADC) pamoja na washiriki mafunzo hayo yaliyofanyika kwa wiki moja mjini Morogoro yakihusisha awamu mbili za waandishi hao.[/caption]

“ Matarajio ni kuona walau kuanzia sasa Televisheni, Redio zote na vyombo vya habari  nchini vinaweka mkazo katika kutoa fursa kwa wataalamu mbalimbali wa Serikali kueleza kuhusu faida za SADC na mchango wa Tanzania katika ustawi wa Jumuiya hiyo na fursa zilizopo” Alisisitiza Dkt.  Abbasi

Alibainisha kuwa matarajio ni kuona vyombo vya habari vikiweka mkazo katika  kuhakikisha kuwa kila mwananchi anaelewa na kutambua wajibu wake katika kipindi chote cha mkutano wa SADC.

Mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wanachama wa SADC utatanguliwa na shughuli mbalimbali  ikiwemo wiki ya viwanda, mkutano wa makatibu wakuu na wataalamu wa sekta mbalimbali na kufuatiwa na ule wa Mawaziri.

  [caption id="attachment_45257" align="aligncenter" width="900"] Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kuandika na kuripoti habari za SADC Eshe Muhiddin akizungumza wakati wa mkutano huo leo Julai 13, 2019 mjini Morogoro , ikiwa ni siku ya kufunga mafunzo hayo.[/caption] [caption id="attachment_45256" align="aligncenter" width="750"] Muwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Ujerumani Bw. Dagmore Tawonezvi akieleza hatua zinazochukuliwa na shirika hilo na matarajio yao waandishi wa habari wa Tanzania baada ya kushiriki mafunzo yakuwajengea uwezo ili waweze kuandika na kuripoti habari zinazohusu jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Hayo yemejiri leo Julai 13, 2019 mjini Morogoro wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo yaliyoshirikisha washiriki zaidi ya 60.[/caption] [caption id="attachment_45259" align="aligncenter" width="900"] Washiriki wa mafunzo yanayolenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kuandika na kuripoti habari za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusinini mwa Afrika (SADC) wakifuatilia mafunzo hayo, Mafunzo yamefanyika kwa wiki moja yakihusisha awamu mbili za waandishi hao, mafunzo hayo yamefungwa leo Julai 13, 2019 na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi.[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi