Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yaombwa Kutekeleza Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa.
Sep 13, 2017
Na Msemaji Mkuu

  [caption id="attachment_13447" align="aligncenter" width="750"] Waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja Utetezi toka taasisi ya Twaweza Bi. Annastazia Rugaba wakati akielezea hali ya upatikanaji wa taarifa Serikalini kuelekea maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kupata taarifa Septemba 28. (Picha na Eliphace Marwa)[/caption]

 Na: Neema Mathias

Wadau  wa Sekta ya Habari  wameiomba Serikali kutekeleza sheria ya upatikanaji wa taarifa kwa lengo la kuwafanya wananchi kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu mambo mbalimbali  yanayoendelea katika serikali yao.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya umuhimu wa upatikanaji wa taarifa kwa wananchi na watafiti mbalimbali katika kuchangia maendeleo na wao wenyewe kunufaika.

[caption id="attachment_13448" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa, Kajubi Mukajanga (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kupata taarifa Septemba 28 na kuiomba Serikali kutekeleza sheria ya kupata taarifa, katikati ni Meneja Utetezi toka taasisi ya Twaweza Bi. Annastazia Rugaba na kushoto ni Meneja Programu wa Baraza la Habari Tanzania(MCT) Bi. Pili Mtambalike.[/caption]

“Sheria ya upatikanaji wa taarifa ni kama sheria mama kwetu kwani inamlenga kila Mtanzania, kupata na kusambaza taarifa ni haki ya kila mtu hivyo ifike mahali tuhakikishe kuwa sheria hii inatendewa haki, tunaiomba serikali iitungie kanuni na ichapishwe rasmi katika gazeti la serikali,” alieleza Bw. Mukajanga.

 Alifafanua kuwa  wakati huu tunapoelekea katika siku ya kimataifa ya upatikanaji wa habari  ambayo hufanyika kila mwaka Septemba, 28, lengo la wadau ni kuhimiza na kuhamasisha uhuru wa watu kupata taarifa pindi zinapohitajika.

 Mukajanga alieleza kuwa wananchi wakipata taarifa wataweza kuchangia ipasavyo  jitihada za   maendeleo na kufichua vitendo viovu vinavyoendelea katika jamii kama rushwa na vitendo vingine  ambavyo vipo kinyume na maadili ya utumishi wa umma. Hatua hii  itaiwezesha serikali kuhakikisha mipango yake inaendana na hali halisi ya jamii husika.

[caption id="attachment_13450" align="aligncenter" width="750"] Meneja Utetezi toka taasisi ya Twaweza Bi. Annastazia Rugaba akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akiiomba Serikali kutekeleza sheria ya kupata taarifa kuelekea maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kupata taarifa Septemba 28, katikati ni Mwenyekiti wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa Kajubi Mukajanga na kushoto ni Meneja Programu wa Baraza la Habari Tanzania(MCT) Bi. Pili Mtambalike.[/caption]

“Kwa sasa kuna uwezekano mkubwa wa wananchi kutopata taarifa wanazozihitaji kwani tafiti za mwezi Januari na  Februari mwaka 2016 zilizofanywa na watafiti wakiwa kama wananchi wa kawaida zinaonesha kuwa walipata suala 1 kati ya 3 ambayo ni sawa na asilimia 33. Watafiti hao walitembelea ofisi 131 za serikali katika wilaya 26 za Tanzania Bara”alifafanua Bw. Mukajanga.

 Kutokana na utafiti uliofanywa kabla ya kupitishwa  kwa sheria hiyo, asilimia 84 ya wananchi waliunga mkono muswada wa upatikanaji wa taarifa bungeni huku  asilimia 77 wakiamini kuwa wananchi wa kawaida wana haki ya kupata taarifa zinazohusu serikali.ambapo asilimia 80 ya wananchi wakiamini kuwa matendo ya rushwa na matendo mengine maovu yatapungua iwapo wananchi watapata taarifa.

[caption id="attachment_13451" align="aligncenter" width="750"] Meneja Utetezi toka taasisi ya Twaweza Bi. Annastazia Rugaba akielezea kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) hali ya upatikanaji wa taarifa Serikalini kuelekea maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kupata taarifa Septemba 28.[/caption]

Kwa upande wake Meneja Utetezi  wa Taasisi ya TWAWEZA Bi Annastazia Rugaba  ameiomba serikali ishirikiane  na wadau katika kuandaa kanuni zinazoratibu utekelezaji wa sheria hiyo na kuitangaza rasmi katika gazeti la Serikali.

“Upatikanaji wa taarifa ni msingi imara katika ujenzi wa jamii ya kidemokrasia na maendeleo endelevu, kupitishwa kwa sheria hii ni moja kati  ya mambo yaliyoainishwa kuwa ya muhimu mwaka 2016 na asasi za kiraia, vyombo vya habari na wananchi,” alisema Bi. Rugaba.

Aidha Bi. Rugaba amewaasa wananchi na waandishi wa habari kuanza kuitumia sheria hiyo kupata taarifa bila kungoja kanuni hizo kwani nchi yetu ni moja kati ya nchi chache zinazotumia  sheria hiyo, hivyo ni vyema kudai taarifa wanazohitaji kwa uhuru.

Amezipongeza ofisi za serikali katika  idara za ujenzi, ardhi na mipango, ambazo katika utafiti uliofanywa ziliongoza  kwa kutoa taarifa huku ofisi za Wakurugenzi wa Wilaya zikitoa taarifa kwa kiwango  cha chini.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi