Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yaandaa Miongozo kwa Mawakala na Waajiri wanaotaka kuajiri watanzania
Sep 05, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_12074" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde akijibu swali wakati wa kikao cha Bunge Leo Mjini Dododma[/caption] [caption id="attachment_12073" align="aligncenter" width="750"] Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongoza kikao cha Bunge leo Mjini Dodoma.[/caption]

Na. Lilian Lundo - MAELEZO - Dodoma.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Balozi za Tanzania zilizopo nchi mbalimbali Mashariki ya Kati imeweka miongozo kwa mawakala na waajiri wanaotaka kuajiri wafanyakazi kutoka Tanzania ili kuziba mianya ya kusababisha Watanzania wanaokwenda kufanya kazi nje ya Tanzania kupoteza haki zao.

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni, Mjini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Asha Abdullah Juma kuhusu wanawake wanaokwenda kufanya kazi za ndani katika nchi za Kiarabu na kufanyiwa ukatili mkubwa.

"Serikali imeweka miongozo itakayosaidia sio tu kuwabana mawakala bali pia kuwasaidia Watanzania kutumia fursa za ajira zilizopo nje ya nchi ili kupunguza tatizo la ajira hadi kwa vijana kwa kuelekeza kila mfanyakazi kuwa na wakala rasmi na kupata mkataba kutoka Ubalozi," amefafanunua Mavunde.

Amesema kuwa ubalozi unakuwa na taarifa katika kila hatua ambayo Watanzania wanapitia wakati wa maandalizi ya kwenda kufanya kazi hivyo kulinda maslahi yao.

Aidha, mwajiri anayetaka kuajiri mfanyakazi kutoka Tanzania atatakiwa kusoma na kuelewa muongozo na baada ya kukubalina nao anatakiwa kujaza fomu ya kuomba kumuajiri Mtanzania na kuwasilisha ubalozini kwa ajili ya kufanyiwa kazi, ambapo maombi hayo yatafuatiwa na mkataba wa kazi.

[caption id="attachment_12075" align="aligncenter" width="750"] Mmoja wa Wabunge wa Viti Maalum Chama cha Wananchi (CUF) akila kiapo leo Bungeni Mjini Dodoma.[/caption]

Mavunde amesema kuwa, mkataba huo una vipengele vikuu vitano ambavyo ni taarifa ya mwajiri, taarifa ya mwajiriwa, mshahara wa mwajiriwa, masharti ya mkataba na maelezo ya mawakala wa Tanzania na Omani. Aidha mwajiri na wakala wanapaswa kukidhi mahitaji hayo ili Serikali itoe idhini kwa Mtanzania aliye tayari kufanya kazi aendelee na taratibu za ajira katika nchi hizo.

Ameendelea kwa kusema kuwa, takwinu zilizopo zinaonesha kuwa Watanzania zaidi ya elfu 12 ambapo ubalozi unawatambua wanafanya kazi katika kada mbalimbali nchini Oman. Kati ya hao wanawake watatu wamepoteza maisha kwa sababu mbalimbali ikiwemo ugonjwa na ajali.

[caption id="attachment_12076" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimpongeza mmoja wa Wabunge wa Viti Maalum kutoka Chama cha Wananchi (CUF) baada ya kula kiapo leo Bungeni Mjini Dodoma[/caption]

Hata hivyo Mavunde amesema katika vifo vilivyowahi kuripotiwa ambavyo Serikali ilifuatilia hadi kujua vyanzo halisi vya vifo hivyo hakuna taarifa kuhusu vifo vilivyosababishwa na mauaji ya makusudi na mara zote Serikali inapopata taarifa za vifo katika nchi hizo hufuatilia kwa kushirikiana na mamlaka za nchi husika kujua hatma za familia zilizopoteza mwenzi wao ikiwa pamoja na malipo ya fidia kutoka kwa mwajiri wa marehemu.

Serikali imekuwa makini katika hatua za awali za maandalizi ya safari hizo kwa kuwabana mawakala na kuhakikisha kuwa mikataba inakuwa ni mizuri ili kuwezesha kuziba mianya yote ya kukwepa majukumu kwa pande zote inayoweza kusababisha Watanzania wanaokwenda kufanya kazi katika nchi hizo kupoteza haki zao.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi