Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yaahidi Kupeleka Gari ya Wagonjwa Hospitali ya Wilaya Manyoni
Oct 30, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_37578" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndugulile akikagua madaftari ya wagonjwa waliolazwa wodi ya akina mama kwenye hospitali ya Wilaya ya Manyoni,kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Bi.Rahabu Solomon[/caption]

Na WAMJW-Manyoni

Serikali imetangaza neema ya kupeleka gari ya  wagonjwa (Ambulance)  katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni ili kutatua tatizo linaloikabidi Wilaya hiyo hususan ya vifo vitokanavyo na uzazi.

Ahadi hiyo imetolewa jana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipoitembelea hospitali hiyo kwa lengo la kutazama utoaji wa huduma za afya ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tatu katika mkoa wa Singida.

Dkt. Ndugulile amefikia uamuzi huo baada ya kusikiliza kero kutoka kwa wananchi wanaotumia hospitali hiyo ambapo wengi walisema kungekuwepo na gari ya wagonjwa kungeepusha vifo vya akina mama wajawazito na watoto pamoja na wagonjwa wanaohitaji huduma za dharura.

"Naomba niwaahidi wananchi wa Manyoni, Serikali imeagiza magari ya kubebea wagonjwa ambayk yanaweza kufika mwezi Disemba mwaka huu,hivyo nitahakikisha katika mgao wa magari hayo basi na hospitali hii ya Wilaya  inapata gari moja kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi wa hapa. Alisema Dkt. Ndugulile.

[caption id="attachment_37579" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwasilikiza watoa huduma katika moja ya wodi zilizopo kwenye hospitalinya wilaya ya Manyoni[/caption] [caption id="attachment_37576" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wananchi waliokuwa wakisubiri huduma wakati alipofanya ziara hospitalini hapo kuona hali ya utoaji wa huduma za afya.[/caption] [caption id="attachment_37577" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (Kulia) akifafanua jambo wakati alipotembelea kitengo cha kuzalisha chakula cha lishe kwa akina mama wajawazito na watoto katika Hospitali ya Mtakatifu Gasper. Kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali hiyo Fr. Seraphine Lesiriam.[/caption]

Aidha, Dkt.Ndugulile aliahidi kuwatafutia wataalam wa Afya watakaoweza kwenda  kupunguza uhaba wa watumishi wanaokabiliana nayo hospitali hiyo

Naye Mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Atupele Mohamed alisema hospitali hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa majengo ikiwemo chumba cha huduma za uzazi ambapo uwezo wake kwa mwezi ni  kuzalisha akina mama 90 lakini kwa sasa huzalisha  wastani wa akina mama 400.

Aidha, Dkt. Atupele alisema Hospitali hiyo ina upungufu mkubwa wa watumishi wenye sifa, ambapo ina jumla ya watumishi 107 sawa na asilimia 53 ya watumishi wanaohitajika.

Dkt. Atupele alitaja   uhaba mkubwa wa watumishi hao  ni Madaktari, Wauguzi, Wataalamu wa mionzi na wataalamu wa kutoa huduma za usingizi.

Katika Wilaya hiyo Naibu Waziri huyo aliweza kutembelea  kutembelea kituo cha kulea wazee na wasiojiweza cha Sukamahela pamoja na Hospitali ya rufaa ya Mtakatifu Gasper iliyopo  Itigi na  kuridhika na hali ya utoaji wa huduma za afya katika Hospitali hiyo.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi