Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali ya Awamu ya Tano Yatekeleza kwa Vitendo Dhana ya Uwezeshaji Wananchi
Mar 06, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_41124" align="aligncenter" width="900"] Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Dkt. Seraphia Mgembe akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mahama Wilayani Chamwino wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo yakuwajengea uwezo wakulima hao zaidi ya 100 waliorasimisha mashamba yao na kupatiwa hatimilki za kimila za kumiliki ardhi zinazowawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi.[/caption]

Na; Frank  Mvungi- Dodoma

Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Mhe. Rais, Dkt.  John Pombe Magufuli imedhamiria kwa dhati kuwawezesha wananchi kujenga uwezo wa kujitegemea kiuchumi tangu ilipoingia madarakani mwaka 2015.

Dhamira hii safi imekuwa ikitekelezwa kwa vitendo   na  Serikali, Tumeshuhudia  Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA)  unavyoendeleza azma hii  kwa kujenga uwezo kwa wananchi ili watumie ardhi kujikwamua kiuchumi kama azma ya ya Serikali yetu ilivyo.

Mpango huu wa MKURABITA umejikita katika kuwawezesha wananchi wanyonge ili waongeze tija na kuchangia katika ujenzi wa uchumi na hasa kujenga Taifa linalojitegemea na lenye wananchi wanaoshiriki kumiliki uchumi unaotokana na rasilimali zilizopo katika maeneo yao.

Jukumu kubwa linabaki kwa wananchi  kuunga mkono Serikali ili juhudi hizi zakuwakwamua kiuchumi  zizae matunda kwa wakati ili Tanzania ifikie azma ya kuwa nchi ya asali na maziwa kama alivyodhamiria Mhe. Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli.

[caption id="attachment_41125" align="aligncenter" width="900"] Meneja urasimishaji ardhi vijijini kutoka Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Bw. Antony Temu akisisitiza jambo kwa washirki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima zaidi ya 100 wa kijiji cha Mahama Wilayani Chamwino wakati wa mafunzo kwa wakulima hao leo.[/caption]

Wananchi katika maeneo mbalimbali hapa nchini wamenufaika na urasimishaji wa ardhi yakiwemo mashamba, kwa mfano katika Wilaya ya Chamwino tumeona uwezeshaji ukifanyika kwa wakulima wa vijiji vya Mahama na Membe, lengo likiwa ni kuwawezesha wananchi hawa kutumia hatimilki za kimila za kumiliki ardhi kujikwamua kiuchumi.

Rai kwa wananchi ni kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano katika jitihada zake za kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi ya kupigiwa mfano kupitia mipango mbalimbali inayotekezwa ukiwemo huu wa urasimishaji rasilimali na biashara za wanyonge.

Mpango huu una faida lukuki kwa wananchi, nampongeza Mhe.  Rais kwa kuendelea kuweka mkazo katika masuala yote yanayolenga kuwawezesha wananchi hasa wanyonge vijijini ili waweze kufurahia na kujikwamua kiuchumi kupitia rasilimali zilizopo ikiwemo ardhi .

Urasimishaji ardhi hasa vijijini ni kichocheo cha maendeleo na umekuwa na faida nyingi, baadhi yake ni kuwasaidia wananchi kuwa na umuliki ardhi unaotambulika kisheria, uhakika wa usalama wa milki ya rasilimali ardhi zinazomilikiwa huko vijijini, kupunguza migogoro ya ardhi, kuongeza thamani ya ardhi husika, kutumia hatimilki za kimila kujipatia mitaji kupitia katika taasisi za fedha.

[caption id="attachment_41126" align="aligncenter" width="900"] Sehemu ya wakulima zaidi ya 100 wa kijiji cha Mahama Wilayani Chamwino wakifuatilia mafunzo yakuwajengea uwezo ili waweze kutumia hatimilki za kimila za kumiliki ardhi kijikwamua kiuchumi baada ya kurasimisha mashamba yao.Faida nyingine ni kuongeza ushiriki wa watanzania walio wengi kwenye mfumo rasmi wa uchumi wa kisasa, hasa wananchiambao awali walikuwa hawajarasimisha mashamba yao au ardhi wanazomiliki.

[/caption]

Kwa upande wake mratibu wa MKURABITA Dkt. Seraphia Mgembe  amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano kupitia mpango huo ni kuhakikisha kuwa inawawezesha wananchi kushiriki katika kujenga uchumi na kuwa na uwezo wa kumiliki rasilimali zilizopo katika maeneo yao.

“ Serikali inatambua umuhimu wa kuwezesha wananchi wake ndio maana imekuja kuwajengea uwezo ili mtumie hatimilki za kimila za kumiliki ardhi kujikwamua kiuchumi kwa kuchukua mikopo katika taasisi za fedha ili muweze kuboresha kilimo cha mazao ya biashara hasa alizeti.” Alisisitiza Dkt. Mgembe

Akifafanua Dkt. Mgembe  amesema kuwa wananchi wanapaswa kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na Serikali kupitia mpango huo  ili kujenga msingi  wa maendeleo endelevu yanayoendana na uchumi wa viwanda.

”Mpango wa matumizi bora ya kijiji cha Mahama wilayani Chamwino umewezesha mashamba 1000 kupimwa na hatimiliki 500 zimeweza kuandaliwa kupitia MKURABITA ili ziweze kuwanufaisha wananchi kiuchumi kwa kuongeza tija katika uzalishaji” Alisisitiza Mhe.  Mwaka.

Aidha , MKURABITA imeweza kuanzisha na kuwezesha utekelezaji wa mfumo shirikishi wa urasimishaji rasilimali vijijini ambao wadau wake muhimu ni wamiliki wa rasilimali zinazomilikiwa katika sekta isiyo rasmi, tunashudia jinsi nguvu kubwa ilivyowekezwa na Serikali ili kuwafanya wananchi wote wanufaike na urasimishaji ardhi na bisahara zao.

Baadhi ya Halmashauri zilizonufaika na Mpango wa urasimishaji ni pamoja na;Chamwino, Musoma,Serengeti, Geita, Kahama, Muleba, Kigoma, Makete, Wete, Nachingwea, Masasi, Kasulu,Mvomero, Singida, Handeni, Bagamoyo, Rufiji, Mkuranga, Sumbawanga, Manyoni, Mpwapwa, Njombe, Bunda, Kilombero, Ludewa, Kilosa, Sikonge, Mbarali, Mbinga, Mpanda, Mufindi, Moshi, Meru, Mwanga, Bunda, Kiteto, Kaskazini A (Unguja) na Mkoani (Pemba)

Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuhakikisha kuwa inaondoa tatizo la kuwepo kwa rasilimali vijijini zinazomilikiwa katika mfumo au sekta isiyo rasmi.urasimishaji umefungua fursa kwa wananchi ili waweze kujenga uchumi na kujitegemea.

     

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi