[caption id="attachment_15674" align="aligncenter" width="750"] Kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kushoto), Kaimu Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, Kamishna Msaidizi wa Nishati-Maendeleo ya Nishati, James Andilile na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt Tito Mwinuka wakiwa katika kikao na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) na watendaji wa Benki ya Dunia (WB).[/caption]
Na: Teresia Mhagama, DSM
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Benki ya Dunia (WB) kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji umeme kutoka Iringa- Mbeya- Tunduma na Tunduma hadi Sumbawanga katika msongo wa kilovolti 400.
Katika kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 Septemba, 2017, ujumbe wa Benki ya Dunia uliongozwa na afisa anayeshughulikia masuala ya nishati nchini, Natalia Kulichenko.
Dkt. Kalemani alisema kuwa endapo taratibu zote zitatekelezwa ndani ya muda wa makubaliano kati ya Benki ya Dunia na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) mradi huo unatarajiwa kuanza mwezi Machi mwaka 2018.
[caption id="attachment_15676" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akiongoza kikao baina ya watendaji wa Wizara, TANESCO na Benki ya Dunia (WB) kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini, jijini Dar es Salaam.[/caption]“Miradi hii ni muhimu sana na hata Mkuu wa nchi anaifuatilia kuhakikisha kuwa inatekelezwa ili kuboresha huduma ya upatikanaji wa umeme kwa wananchi wetu hivyo ni muhimu kwa pande zote tujadiliane masuala yatakayopelekea mradi kuanza mwezi Machi mwakani,” alisema Dkt. Kalemani.
Dkt. Kalemani aliongeza kuwa mradi huo wa miundombinu ya usafirishaji umeme wa msongo wa kilovolti 400 utakaotekelezwa ndani ya miezi 18 utaimarisha hali ya upatikanaji wa umeme katika mikoa husika.
Aidha aliwaagiza watendaji wa TANESCO kuhakikisha kuwa wanatekeleza masuala mbalimbali ndani kwa wakati ikiwemo uhuishaji wa taarifa ya tathmini ya athari za kimazingira na utangazaji wa zabuni ya mradi huo.
[caption id="attachment_15677" align="aligncenter" width="750"] pic mojaNaibu Waziri Dkt. Kalemani alitumia fursa hiyo pia kuishukuru Benki ya Dunia kwa kukubali kufadhili mradi huo na miradi mbalimbali ya umeme ikiwemo mradi mkubwa wa miundombinu ya usafirishaji umeme katika msongo wa kilovolti 400 kutoka Iringa hadi Shinyanga ambapo Benki hiyo ilitoa fedha za utekelezaji wa mradi katika kipande cha Iringa- Dodoma.
“Mradi huu ambao umekamilika mwaka jana umeleta manufaa makubwa kwani umeongeza uwezo wa kusafirisha umeme kutoka Kanda ya Kusini Magharibi ambako kuna vyanzo vingi vya umeme na kupeleka Kanda ya Kaskazini na Kaskazini Magharibi ambako kuna shughuli nyingi za kiuchumi na wananchi wanapata umeme wa uhakika,” alisema Dkt Kalemani.
Kwa upande wake, Bi Natalia Kulichenko alimueleza Naibu Waziri kuwa Benki hiyo ipo tayari kushirikiana na Wizara pamoja na TANESCO katika kutekeleza masuala mbalimbali yatakayopelekea mradi huo kutekelezwa kama ilivyopangwa.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na TANESCO. Miongoni mwao ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Dkt. Juliana Pallangyo, Kaimu Mkurugenzi wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka na Kaimu Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga.