[caption id="attachment_36989" align="aligncenter" width="800"] Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw.Patrick Golwike akifungua kikao kazi cha Kamati Tendaji ya Taifa ya ulinzi wa Wanawake na Watoto walipokutana kujadili Muongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) 2017/18-2021/22, kilichofanyika Oktoba 17, 2018 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma, kulia kwake ni Katibu wa Kamati hiyo Bw.Mwambene Atupele.[/caption]
Na. Mwandishi Wetu
Serikali imedhamiria kumaliza changamoto za ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto kwa kushirikia na wadau wanaohusika na masuala ya wanawake na watoto nchini.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw.Patrick Golwike alipokuwa akifungua kikao kazi cha Kamati Tendaji ya Taifa ya ulinzi wa wanawake na watoto kilichofanyika Oktoba 17, 2018 Jijini Dodoma kujadili utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya makundi hayo.
[caption id="attachment_36990" align="aligncenter" width="800"] Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Uratibu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Joseph Kiraia akichangia hoja wakati wa kikao kazi cha Kamati Tendaji ya Taifa ya ulinzi wa wanawake na watoto walipokutana kujadili Muongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_36991" align="aligncenter" width="800"] Mratibu wa MTAKUWWA Bw.Seto Ojwando akiwapitisha wajumbe katika Mwongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) wakati wa kikao kazi hicho.[/caption]Kamati hiyo imekutana kujadili Utekelezaji wa Mpango Kazi huo unaolenga kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) na changamoto zinazotokana na vitendo hivyo.
Aidha, Miongoni mwa maeneo muhimu yaliyojadiliwa katika mpango kazi huo ni pamoja na kuhakikisha maeneo nane ya kimkakati yanafikiwa ili kufukia malengo ya kupunguza aina zote za ukatili kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2020, na kuwataka wadau wote kushirikiana katika kukabiliana na vita ya ukatili kwa wanawake na watoto.
Maeneo ya utekelezaji yaliyoainishwa ni pamoja na; uimarishaji wa uchumi wa Kaya, kupinga mila na desturi zinazomkandamiza mwanamke na mtoto, kuhakikisha mazingira salama sehemu za umma, kuimarisha mahusiano mema na kuziwezesha familia katika malezi bora, utekelezaji na usimamizi wa sheria, utoaji huduma kwa waathirika wa ukatili pamoja na mazingira salama shuleni na stadi za maisha.
[caption id="attachment_36992" align="aligncenter" width="800"] Mratibu wa Taifa wa Dawati la Jinsia na Watoto Bi.Happiness Mugyabuso akinukuu hoja zinazowasilishwa na wajumbe wa kikao kazi cha Kamati Tendaji ya Taifa ya ulinzi wa wanawake na watoto walipokutana kujadili Muongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (hawapo pichani) walipokutana Oktoba 17, 2018 Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_36993" align="aligncenter" width="800"] Mratibu Taifa wa Masuala ya watoto kutoka World Vision Bi.Akwelina John akichangia jambo wakati wa kikao kazi hicho[/caption] [caption id="attachment_36994" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mada zilizowasilishwa wakati wa kikao kazi hicho.[/caption]“Wajibu wa wadau wote wenye kutekeleza afua za kuzuia na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kutumia mwongozo huu katika maeneo mnayosimamia kwani utarahisisha katika utekelezaji wa majukumu yetu na kuhakikisha maeneo nane yaliyoainishwa yanafikiwa kikamilifu”.Alisisitiza Golwike
Aliongezea kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali katika kukabiliana na vitendo vya ukatili nchini kupitia Sera, Sheria, Kanuni, Miongozo na Mipango ya Kisekta ikiwemo uanzishwaji wa madawati ya Jinsia na watoto katika kila Wizara na katika vituo vya polisi 417, kuandaliwa kwa sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia (2000) na Sera ya Mtoto ya mwaka 2008.
Jitihada nyingine ni pamoja na uanzishwaji wa mifumo ya ulinzi wa mtoto katika Halmashauri 63 nchini pamoja na uanzishwaji wa Mahakama za kusimamia kesi za watoto katika Halmashauri 131.
[caption id="attachment_36995" align="aligncenter" width="800"] Katibu wa Kamati hiyo Bw.Mwambene Atupele akifafanua jambo wakati wa kikao kazi hicho.[/caption] [caption id="attachment_36996" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya wajumbe wakifuatilia uwasilishaji wa hoja kutoka kwa Mwenyekiti wa kikao kazi hicho Bw. Patrick Golwike.[/caption] [caption id="attachment_36997" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Taifa ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto Bw.Patrick Golwike (Wa tano kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati hiyo mara baada ya ufunguzi wa kikao kazi cha kujadili Muongozo wa Uratibu wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) 2017/18-2021/22, kilichofanyika Oktoba 17, 2018 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.(Picha Zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)[/caption]Kwa upande wake Mratibu wa Taifa wa Dawati la Jinsia na Watoto Bi.Happiness Mugyabuso aliongezea kuwa ili kufikia malengo ya kutokomeza ukatili kwa makundi hayo ni vyema mpango kazi huo ukatekelezwa kwa vitendo ili kutorudisha nyuma jitihada za Serikali.
“Ni vyema sasa mpango kazi huu ukajadiliwa kwa kina ili kufikia malengo na kuwa miongozo mizuri itayotoa utaratibu wa uratibu, usimamizi na ufuatiliaji”.alisistiza Mugyabuso
Aidha, alieleza kuwa wadau wanaotekeleza mpango huu ni pamoja na Wizara, Idara na Wakala za Serikali, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa wanaoshughulikia masuala ya wanawake na watoto, Mashirika ya Kimataifa , Asasi zisizo za Kiserikali, Sekta Binafsi, Taasisi za Dini na Wanawake kwa pamoja wamekuwa ni chachu katika vita dhidi ya ukatili kwa wanawake na watoto nchini.