Na Tiganya Vincent - Sikonge
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imeliagiza Jeshi la Polisi mkoani hapo kuanza mara moja kuendesha zoezi la ukaguzi wa magari yote yanayotoa huduma za usafirishaji wa abiria kwa ajili ya kuhakikisha kuwa yaliyo mabovu yasiamishwe kutoa huduma hiyo ili kuzuia ajali zinazotoka na ubovu wa vyombo hivyo.
Kauli hiyo ilitolewa jana wilayani Sikonge kufuatia ajali mbili za Basi la Kampuni ya Adventure lilisababisha kifo cha mtu mmoja na la Kampuni ya HBS zilizotokea hivi karibuni.
Alisema kuwa baada ya kuangalia gari la HBS lenye namba T960 AHH bodi lake lilionekana limechakaa lakini liliendelea kutoa huduma ya usafiri.
Kufuatia dosari hiyo ilionekana katika Bodi ya Basi hilo alimwagiza Kamanda wa Polisi Usalama wa Barabarani Mkoa wa Tabora (RTO) kuanza mara moja ukaguzi wa maagari yote ya abiria siku zote badala ya kugonja wiki ya usalama wa barabarani ndio zoezi hilo ufanyike.
Mwanri aliongeza kuwa haiwezekani magari mabovu yaendelee kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria huku maisha ya watu yakiendelea kupoteza kwa sababu ya ajali zinazosababishwa na ubovu wa magari.
Alisisitiza kuwa gari lisiruhusiwe kusafiri likiwa bovu hadi hapo litakapofanyiwa maboresho ya kuondoa ubovu uliopo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres ajali ya basi la HBS ilisababishwa na uzembe wa Dereva wa gari hilo ambaye alijaribu kulipita gari jingine katika upande usio ruhusiwa na kujikuta akiongia katika daraja na basi kupinduka.
Alisema kuwa tukio lilisababisha abiria zaidi ya 20 kujeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Sikonge.
Mmoja wa Majeruhi wa gari HBS Bibi Sada Shabani alikiri Dereva wa gari lao kutokuwa makini wakati alipokuwa anapishana na gari jingine na kujikuta akiingia katika daraja na kujikuta likipinduka.
Alisema kuwa ajali hiyo ingeweza kuepukika kama dereva huyo angesubiri lori la mafuta lipite na yeye ndiye aendelee na safari yake.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa aliagiza Jeshi la Polisi kuwatafuta Madreva wa mabasi yote mawawili waliosababisha ajali ya kisha kukimbia ili wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Tabora amemwagiza Mganga Mkuu wa Wilaya ya Sikonge kuhakikisha mikanda(film) kwa ajili ya kuchukua picha inayoonyesha ugonjwa mtu inaagizwa haraka kwa ajili kutoa huduma kwa mmoja wa majeruhi wa ajali iliyosababishwa na basi la Adventure ambaye hadi hivi sasa anasubiri kuangalia ni kwa kiasi gani ameumia kifua.
Alisema kuwa ni uzembe wa hali ya juu mgonjwa kushindwa kupata huduma kwa zaidi ya siku tatu kwa sababu ya kukosekana kwa mikanda ya kuchukua picha ili kujua ameumia kwa kiasi gani ambayo inapatikana Tabora mjini katika ofisi za MSD.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa kama wanaona kuwa wameshindwa kumpatia huduma hiyo ni vema wakamsafirisha kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kitete ili apate huduma hiyo mapema.