Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Apongezwa kwa Kuwezesha Wanyonge
Nov 18, 2018
Na Msemaji Mkuu

Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania   (MKURABITA) Bi. Seraphia Mgembe akizungumzia faida za mafunzo waliyopata  Wajasiriamali zaidi ya 700 wa mjini Njombe yakilenga kuwajengea uwezo  ili warasimishe Biashara zao na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi.

Na ; Frank Mvungi- Njombe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amepongezwa kwa  kuendelea kuwawezesha wajasiriamali  kupitia Mpango wa Kurasimisha  Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) .

Akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku 10 kwa wajasiriamali zaidi ya 700 wa  Mjini Njombe Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Christopher Ole Sendeka amesema kuwa swala la urasimishaji Biashara kwa wajasiriamali ni takwa la Kisheria na pia ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ibara ya 58 ambapo Biashara zote zinatakiwa  kuendeshwa katika mfumo rasmi na Serikali ya Awamu ya Tano imeweka mkazo mkubwa ili kuwainua wajasiriamali wanyonge.

“ Nawapongeza MKURABITA na Halmashauri ya Mji wa Njombe kwa kufanikisha mafunzo haya kwa wajasiriamali yanayolenga kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha Biashara zao na pia kuanzishwa kwa Kituo Kimoja cha Urasimishaji Biashara hapa Njombe itakuwa ukombozi kwa wajasiriamali wetu”; Alisisitiza Ole Sendeka.

[caption id="attachment_38373" align="aligncenter" width="900"] Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka akifunga mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 700 wa Mjini Njombe yaliyoratibiwa na Ofisi ya Rais, Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) yakilenga kuwajengea uwezo wajasiriamali hao ili waweze kurasimisha Biashara zao. Hayo yamejiri leo tarehe 17/11/2018 Mjini humo.[/caption]

Akifafanua Mhe.  Ole Sendeka amesema kuwa kuanzishwa kwa Kituo cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara  Mjini Njombe kumewashirikisha wadau kama MKURABITA,  TRA, SIDO na Benki mbalimbali ikiwa ni sehemu ya   juhudi za Serikali kukabiliana na tatizo la Ongezeko la Biashara ndogo na za kati zisizo rasmi na ambazo zinakuwa kwa kasi.

Aliongeza kuwa wananchi wote wanajukumu kubwa la kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto zilizopo katika maeneo yao hasa kwa wajasiriamali kuhakikisha kuwa wanatoa taarifa za wale wote wanaotaka kukwamisha juhudi za Serikali zinazolenga kuwainua.

Kwa upande wake Mratibu wa MKURABITA Bi. Seraphia   Mgembe amesema kuwa washiriki wa mafunzo hayo wamejengewa uwezo katika maeneo yafuatayo; Urasimishaji na Usajili wa majina ya Biashara, Upatikanaji wa leseni za Biashara na faida zake, utunzaji wa kumbukumbu za Biashara na umuhimu wake, huduma kwa mlipa kodi, Huduma za mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Mbinu za Masoko.

Aliongeza kuwa wajasiriamali wakirasimisha Biashara zao watakuza mitaji yao na kupanua masoko kwa kuwa watakuwa na uwezo wa kukopa katika Taasisi za fedha yakiwemo mabenki.

Sehemu ya Wajasiriamali hao zaidi ya 700 wa Mjini Njombe wakifuatilia hafla ya ufungaji mafunzo hayo iliyofanyika mjini humo ambapo Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Christopher  Ole Sendeka alikuwa mgeni rasmi. Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wajasiriamali hao ili waweze  kurasimisha Biashara zao.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Ruth Msafiri amesema kuwa wajasiriamali wanapaswa kujenga utamaduni wa kurejesha kwa wakati mikopo wanayokopa katika kupitia Taasisi za fedha ili waweze kukuza Biashara zao.

Pia alishauri  Halmashuri  kuangalia namna Bora yakuwawezesha wajasiriamali wanaoanza Biashra ili kuweka utaratibu utakaosaidia kukuza Biashara zao.

Mafunzo yakuwajengea uwezo wajasiriamali yamefanyika Mkoani  Njombe yakilenga kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha biashara zao na kuchangia katika kukuza uchumi. Wajasiriamali zaidi ya 700 wameshiriki katika mafunzo hayo ya siku 10.

 

Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania   (MKURABITA) Bi. Seraphia Mgembe akizungumzia faida za mafunzo waliyopata  Wajasiriamali zaidi ya 700 wa mjini Njombe yakilenga kuwajengea uwezo  ili warasimishe Biashara zao na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi.

Mmoja wa wajasiriamali walinufaika na mafunzo yakuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha Biashara zao Bw. Lucas Kawongo akifurahia cheti alichotunukiwa  na Mkuu wa Mkoa wa Njombe wakati akifunga  mafunzo kwa wajasiriamali  zaidi ya 700 wa Mjini  Njombe. Mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha wajasiriamali kurasimisha  Biashara zao.

Mhasibu wa Mapato kutoka Halmashauri ya Mji wa Njombe Bw.  George C. Mwasera akipokea cheti cha kuhitimu mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais- MKURABITA yakilenga kuwajengea uwezo wajasiriamali ili warasimishe Biashara zao.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher  Ole Sendeka akiwasili  ukumbini kufunga mafunzo kwa  wajasiriamali zaidi ya 700 yaliyoandaliwa na MKURABITA yakilenga kuwajengea uwezo wajasiriamali hao ili warasimishe biashara zao.

(Picha zote na MAELEZO, Njombe)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi