Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira kilichotokea leo tarehe 22 Julai, 2021 katika hospitali ya Rufaa ya Mount Meru mkoani Arusha alipokuwa akipatiwa matibabu.
Mhe. Rais Samia amesema amepokea taarifa za kifo cha Mhe. Anna Mghwira kwa majonzi na masikitiko makubwa hasa akikumbuka mchango wake mkubwa alioutoa katika ujenzi wa taifa.
Amewaomba wanafamilia wote wawe na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na amemuombea marehemu Anna Mghwira apumzike mahali pema peponi, Amina.
Jaffar Haniu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.