[caption id="attachment_46151" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika(SADC) ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, akihutubia wakati wa kufunga Mkutano wa Wakuu wa Nchi za SADC uliofanyioka Jijini Dar es Salaam, Tanzania.[/caption]
Na Judith Mhina
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefungua Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi za Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika- SADC leo Jijini Dar-es-Salaam katika ukumbi Mkutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Akifunga Mkutano huo Rais Magufuli amesema “Rais wa Kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Nyerere alijitoa muhanga na kutoa upendo wake mkubwa kwa nchi za Kusini mwa Afrika na wale wote waliokuwa wanateseka na ukoloni duniani”
Akionyesha furaha yake kwa lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi katika nchi za SADC Rais Magufuli amesema “Kuchukuliwa lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya SADC tumefuta machozi ya Baba wa Taifa Julius Nyerere”
Baba wa Taifa hili aliwapenda watu wake na majirani zake kwa upendo wake mkubwa, alitoa sehemu ya nchi yake katika mikoa tofauti ili Wapigania Uhuru waweze kukaa, kuishi, kujifunza mambo mbalimbali yakiwemo ya kivita na maarifa ili kuzikomboa nchi zao.
Mwalimu alitoa eneo lililojulikana kama Farm 17 kuIe Nachingwea walipoishi wapigania uhuru wa Flerimo ,Mgagao Iringa walipoishi ANC, PAC, Bagamoyo Kaole waliishi wapigania uhuru wa ZANU, ZAPU, ANC, hata Rais wa Zimbabwe wa sasa aliishi hap, eneo la Kongwa ambapo ilikuwa Kambi kubwa na karibu vyama vyote vya ukombozi viliishi hapo.
Akidhibitishwa kuishi kwa Wapigania uhuru hao, Rais Magufuli amesema kuwa ziara aliyoifanya juzi kule Mazimbu Morogoro Rais wa Jamhuri ya Africa ya Kusini Cyril Ramaphosa amekwenda kushuhudia eneo waliloishi, kuzuru makaburi ya Wapigania uhuru waliokufa wakati wa kutafuta uhuru wa nchi yao na pia alikutana na watoto ambao baba yao alikuwa mpigania uhuru na kuwajulisha watoto hao moja ya makaburi ya hapo mazimbu lipo la baba yao.
“Huyu Baba Mwalimu Nyerere hakika alijitoa kwa upendo mkubwa sana ambao siwezi hata kuuelezea”
Mwaka 1975 Jamhuri ya Shelisheli ilipata misukosuko walikwenda kutuliza hali hiyo ni Jeshi la Wananchi wa Tanzania-JWTZ, wakiongozwa na Brigedia Generali Hassan Ngwilizi ambaye walipofanikiwa kudhibiti Mapinduzi haramu alikaa kwa siku kadhaa kama Rais wa Shelisheli hayo mi maagizo ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kama hiyo haitoshi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo JWTZ wameshiriki mara kadhaa kwa miaka tofauti kudhibiti machafuko na hadi leo wako huko kwa ajili ya kulinda usalama wa Raia na mali zao.Hali kadhaliko nchi ya Jamhuri ya Comoros Tanzania ilishiriki kuzima Mapinduzi yaliyofanyika na kurejesha utawala wa kiraia. Yote hayo yamefanyika kwa sababu wa upendo wa Mwalimu Julius Nyerere.
Rais Magufuli amesema Wapigania uhuru wote walioishi Tanzania ambao wako sasa kwenye nchi zao wanajua lugha ya Kiswahili, hivyo Kiswahili ni lugha ya ukombozi amani upendo na mshikamano. Hata Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliitumia kuunganisha watu kwa pamoja na kutafuta uhuru wa Tanganyika ambao ulipatikana kwa kuweka hoja mezani.
Hivyo napenda kuwashukuru Wakuu wa Nchi wote kwa kuwa na sauti moja ya kuunga mkono Kiswahili kuwa lugha ya nne ya nchi wananchama wa SADC. Lugha zinazotambulika ni Kiingereza, Kireno, Kifaransa na Kiswahili lugha ya nne.
Aidha Rais Magufuli amesema Mkutano wa 39 wa SADC umekuwa wa mafanikio sana na umeendeshwa kwa utulivu , upendo na mshikamano wa hali ya juu. Lakini ni kweli yapo mambo ambayo tulitofautiana lakini tuliweka hoja mezani tukajadiliana na kupata jibu la pamoja kama SADC.
Ajenda nyingine zote zimeisha kwa mafanikio kama kauli mbiu yetu inavyosema “Mazingira Wezeshi kwa Maendeleo Jumuishi na Endelevu ya Viwanda, Ongezeko la Biashara na Ajira Kikanda”.kwa pamoja tumepitisha kauli mbiu hiyo na sasa tuko tayari kwa utekelezaji wake.
Kama Mwenyekiti nimepokea taarifa ya Organ ya Wakuu wa Nchi za SADC, kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Namibia Mhe. Dkt Hage Geingob na Organ ya Ulinzi na Usalama kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe Edgar Lungu.
Bado SADC inafatilia suala la Ulinzi na Usalama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Nchi ya Lesotho inatakiwa itungaji wa Taasisi muhimu ya kisheria National Reform Authority , vilevile kuwa na chombo cha SADC kinachokabiliana na majanga kama vile mafuriko, ukame, vimbunga na mambo kama hayo.
Akiongelea taarifa ya hali ya uchumi nchi za SADC, Rais amesema kutokana na matukio ya maafa yaliyoikumba Kusini mwa Afrika hali ya chakula haikuwa nzuri, ambapo ilisababishwa na mafuriko vimbung’a hali ya mabadiliko ya tabia nchi na hali ya uchumi duniani. Hivyo tukaona ni vema kujielekeza kwenye miundombinu, kuboresha rasimu ya uchumi na fedha, uhamasishaji na matumizi sahihi ya rasilimali na fedha zetu.
Akiongelea suala la Jamhuri ya Burundi kujiunga na Nchi wanachama wa SADC,suala limepokelewa ila bado kuna mambo ya msingi ambayo nchi ya Burundi inatakiwa kuyafanya kwanza kabla ya kukubaliwa kujiunga na SADC.
Kama viongozi wa SADC, tumekubaliana kwa kauli moja nchi ya Jamhuri ya Zimbabwe wakati umefika kuondolewa vikwazo, kwa hiyo kila nchi mwanachama atatumia balozi zake zilizo nje ya nchi katika kuhakikisha tunafikisha ombi letu la nchi ya Zimbabwe kuondolewa vikwazo vya kiuchumi.
Pia, nitoe shukurani zangu za dhati kwa mashirika ya Maendeleo ya Kimataifa tunayoshirikiana nayo mwaka 2019/2020 watatupatia Trilioni 74 31 na milioni43 fedha za Euro zitakazotumika kwa shughuli za maendeleo kwa nchi wanachama.
Akikumbusha maadhimisho muhimu mwaka huu ya Miaka 20 bila Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere Rais Magufuli amesema Naomba niwakumbushe nukuu ya Mwalimu Nyerere aliyoitoa mwaka 1997 katika Bunge la Jamhuri ya Afrika ya Kusini.
“Kila nchi inapaswa kuchunga raia wake na rasilimali ili kujiletea maendeleo, hiyo haitoshi ni vizuri kushirikiana na nchi nyingine ili kuleta maendeleo kwa nchi zetu” Julius Nyerere.
Hivyo nchi ya Tanzania itashirikiana na nchi zote Amesema Rais Magufuli.
Pia, mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi kwa nchi zza Jamhuri ya Botswana, Msumbiji, Namibia na Mauritius nawaahidi tutashirikiana nao kama SADC kuangalia uchaguzi huo na kufata vigezo vyote vya SADC. Nawatakia uchaguzi wa amani na msisahau kuzingatia vigezo vya uchaguzi vya sadc.
Mwisho alimalizia na kuwashukuru nchi wananchama wa SADC, kwa kuniamini na kunikabidhi Uenyekiti vilevile nachukua fursa hii kumpongeza Mwenyekiti aliywpita Rais wa Jamhuri ya Namibia, yale yote waliotuachia tutayatekeleza kwa uaminifu kabisa. Pia Namhukuru Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Emason Mnangwaga aliyokuwa anaongoza Taasisi muhimu ya Siasa Ulinzi na Usalama kwa utendaji wao uliotukuka.
Naye Raiswa Jamhuri ya Msumbiji Philipe Nyusi akitoa neon la shukurani amemsifu Rais Magufuli kwa kuendesha kikao chake cha kwanza kama Mwenyekiti kwa uzoefu wa hali ya juu. Pia amemshukuru kwa mapokezi makubwa aliyoyapata yeye binafsi wakati alipofika hapa nchi. Hivyo kwa niaba ya watu wa Msumbiji anaona fahari kuwa sehamu ya Watanzania na anasema asante sana.
Naye Katibu Mtendaji wa SADC Mhe. Dr, Stegomena Tax alisaini makubaliano ya kupata fedha kutoka kwa nchi washirika wa maendeleo wa Jumuiya ya Ulaya ya Euro milioni 43 na Balozi wa Jumuiya ya Ulaya Nchini Botswana Mhe. Jan Sadek mbele ya Marais wa SADC.
Aidha, Dr. Tax amemalizia mkutano huo kwa kuwasilisha Maazimio 38 aliyoyasoma. Ambapo azimio la mwisho ni kuwajulisha wajumbe kuwa Mkutanno ujao wa 40 wa nchi wanachama wa SADC utafanyika nchini Msumbiji.