Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Awabadili Vituo vya Kazi Wakuu wa Wilaya Wawili
Aug 14, 2020
Na Msemaji Mkuu

Ikulu, Chamwino.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko ya vituo vya kazi kwa Wakuu wa Wilaya 2 kama ifuatavyo;

Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemhamisha kituo cha kazi aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Rorya Mkoani Mara Bw. Simon Kemori Chacha, kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma.

Pili, Mhe. Rais Magufuli amemhamisha kituo cha kazi aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Chemba  Mkoani Dodoma Bw. Simon Ezekiel Odunga, kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rorya Mkoani Mara.

Mabadiliko ya vituo vya kazi kwa Wakuu wa Wilaya hao yanaanza leo tarehe 13 Agosti, 2020.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Chamwino

13 Agosti, 2020

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi