Ikulu, Chamwino.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Julai, 2020 amemteua Bw. Gabriel Pascal Malata kuwa Wakili Mkuu wa Serikali (Solicitor General)
Kabla ya uteuzi huo Bw. Malata alikuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali na anachukua nafasi ya Dkt. Julius Clement Mashamba.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Boniface Luhende kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali (Deputy Solicitor General).
Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Luhende alikuwa Mhadhiri katika Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Bw. Gabriel Pascal Malata ambaye ameteuliwa kuwa Wakili Mkuu wa Serikali.
Uteuzi wa viongozi hao unaanza leo tarehe 10 Julai, 2020.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chamwino
10 Julai, 2020