Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Arejea Nchini Kutoka Nchini Zimbabwe
May 30, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_43731" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Brigedia Jenerali Abdallah M. Alphonce na wafanyakazi wa ubalozi huo Bi. Alice Madelena Bi Joyce Makoye katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Mugabe jijini Harare, kabla ya kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kurejea nyumbani akitokea Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi[/caption]

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 30 Mei, 2019 amerejea hapa nchini akitokea nchini Zimbabwe ambako amefanya Ziara Rasmi ya siku 3 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe, Mhe. Emmerson Mnangagwa.

[caption id="attachment_43732" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiteremka kutoka katika ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Alhamisi Mei 30, 2019 akitokea Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril
Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi.[/caption]

Kabla ya kufanya ziara nchini Zimbabwe, Mhe. Rais Magufuli amefanya ziara nchini Afrika Kusini ambako pamoja na kuhudhuria sherehe za uapisho wa Rais wa Awamu ya Tano wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa amefanya mazungumzo na kiongozi huyo, Ikulu Jijini Pretoria.

Baadaye, Mhe. Rais Magufuli akaelekea nchini Namibia ambako amefanya Ziara ya Kitaifa kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo, Mhe. Dkt. Hage Geingob ambapo pamoja na kufanya nae mazungumzo alifungua mtaa mkubwa uliopatiwa jina la Baba wa Taifa la Tanzania Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na pia alitembelea eneo walipozikwa mashujaa wa ukombozi wa Namibia na kiwanda cha nyama cha Meatco.

[caption id="attachment_43733" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna wa Polisi Diwani Athumani baada ya kutelemka kutoka katika ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo alhamisi Mei 30, 2019 akitokea Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi.[/caption]

Alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Mhe. Rais Magufuli amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda na Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakiongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jen. Venance Mabeyo.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

30 Mei, 2019

[caption id="attachment_43734" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo alhamisi Mei 30, 2019 akitokea Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya
ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda[/caption] [caption id="attachment_43735" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe Mhe. Dkt. Emmerson Mnangagwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Mugabe jijini Harare leo alhamisi Mei 30, 2019 baada ya kuhitimisha ziara yake ya Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo
Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi