Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Apokea Bilioni 3 Kutoka Barti Airtel Baada ya Makubaliano Kati ya Serikali na Kampuni Hiyo Kumalizika
Jun 11, 2019
Na Msemaji Mkuu

Na. Paschal Dotto-MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli amepokea kiasi cha Tsh.Bilioni tatu kutoka kampuni ya Barti Airtel, baada ya mazungumzo na makubaliano ya kimaslahi kati ya kampuni hiyo ya simu na Serikali, fedha hizo kuanzia mwezi wa nne, wa tano na wa sita.

Akizungumza  Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais alisema kuwa amefurahishwa na kitendo cha watanzania waliokuwa kwenye kamati ya mazungumzo kwani wamefanya Tanzania kupata mslahi mapana katika uwekezaji wa kampuni hiyo.

“Tumeingia kwenye mazungumzo kati ya kampuni ya simu ya Barti Airtel na ninyi watanzania wazalendo, mlifanya mazungumzo usiku na mchana, mlitumia elimu yenu mliyopewa na mungu na mazungumzo yenu yakafikia mahali mkakubaliana  kwa hiyo nawapongeza ninyi na kampuni ya simu ya Airtel kwa kukubaliana katika hili hongereni sana”, Rais Magufuli.

Rais Magufuli alisema kuwa katika fedha zitakazokuwa zinaingia ambazo ni bilioni Moja kila mwezi zitakwenda kuwasaidia watanzania kwenye miradi mbalimbali, ambayo itakuwa inatoa huduma kwa wananchi wote.

“Fedha zitakazokuwa zinalipwa ambazo ni Tsh Bilioni moja kila mwezi kwa muda wa miaka mitano maana yake kwa mwaka ni bilioni 12, kwa miaka mitano bilioni 60 zitasaidia sana kuboresha huduma za kijamii, mfano ukijenga vituo vya afya vya milioni 500 kama vile vilivyojengwa vitakuwa ni vituo 120, lakini ukiamua kujenga vya milioni 400 maana yake ni vituo 150”, Rais Magufuli.

Rais Magufuli alisema kuwa Tanzania imeingia kwenye historia kwa kufanya makubaliano yaliyodumu kwa takiribani mwaka mmoja na sasa wamekubaliana kuwa kampuni hiyo ya simu itakuwa inatoa Tsh.Bilioni moja kila mwezi kwa miaka mitano, kuongeza umiliki wa hisa kutoka asilimia 40 hadi 49,na kutoa gawio kwa kila faida watakayokuwa wanaipata, kufuta deni la bilioni 930 ambalo Serikali ilitakiwa ilipe.

Aidha Rais Magufuli aliwapongeza kampuni ya Airtel kwa kuweka mbele maslahi ya watanzania kwani tangu kampuni hiyo ianzishwe miaka 19 iliyopita Tanzania haikuwa inapata chochote lakini sasa hivi wameingia makuibaliano ambayo kuitakuwa na maslahi kwa pande mbili.

“kitendo hiki mimi naona kimeshikwa mkono na Mungu kwa sababu katika kipindi cha nyuma tangu Airtel imeundwa miaka 19 katika miaka hiyo yote Serikali ilikuwa inapata sifuri, lakini pia hatukupata gawio lolote na huo ndiyo ukweli, miaka 19 yote imepita bure katika biashara hii, pamoja na kwamba tulikuwa na Asilimia 40 kwenye umiliki wa hisa lakini bado hatukupata chochote, na pia tubandikiwa deni la bilioni 930”, Rais Magufuli.

Rais Magufuli pia alisema kuwa katika mazungumzo hayo amempongeza Mwenyekiti wa Airtel, Sunil Mittal ambaye amekuwa na moyo wa pekee katika kuwezesha makubaliano na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kufanya naye biashara, lakini pia alimshukuru kwa kutoa mchango wa dola za kimarekani milioni Moja ambazo zitaenda kujenga Hospitali ya Uhuru Jijini Dodoma.

Aidha, Rais Magufuli aliwaapisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Edwin Mhede na Katibu Tawala Mkoa wa Njome, Charles Kichele, na kuwataka wakafanya kazi kwa kuleta matokea kwa watanzania.

“Watanzania wanataka kuona matokeo, tutaambizana maneno mazuri lakini hayasaidii, sisi tunataka matokeo mazuri na mimi jukumu langu ni kuteua ili kusudi kiu ya watanzania ikaweze kutimia katika kupata maendeleo”, Rais Magufuli.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.Palamagamba Kabudi ambaye pia alikuwa  Mwenyekiti wa Timu ya mazungmzo kutoka Tanzania, alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeweka historia tangu Serikali ilipoamua kuchukua Maamuzi magumu kwenye kupitia mikataba mablimbali ikiwemo ya Madini pamoja na Mawasiliano .

“Mhe. Rais Naitafakari sana siku hii ya leo yenye mafanikio makubwa kwa Serikali ya Awamu ya Tano, toka ilipochukua maamuzi ya kupitia mikataba mbalimbali ya uwekezaji ikiwemo na huu ambao umetuweka hapa, uliagiza na kuunda timu ya kufuatilia mkataba wa uwekezaji wa Kampuni ya simu ya Barti Airtel na tulifanya na kufanya mazungumzo tulifanya hivyo na leo unapokea matunda yake”, alisema Prof.Kabudi.

Prof.Kabudi alisema kuwa Tarehe 15 Januari 2019, mkataba wa Makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Simu Airtel ulisainiwa na kuzaa matunda yafuatayo, kuongeza umiliki wa hisa kutoa asilimia 40 mpaka asilimia 49, kubadilisha muundo wa bodi huku Mwenyekiti wa Bodi na Mkuu wa Ufundi kuteuliwa na Serikali, Airtel kulipa Bilioni moja kila mwezi kwa muda wa miaka mitano, Airtel kutoa gawio kwa Serikali, Airtel kufuta imefuta deni la Tsh bilioni 937 na kuokoa bilioni 459.13 ambazo zililipwa na Serikali kama Mwanahisa.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Philip Mpango alisema kuwa uamuzi huo wa makubaliano kati ya Serikali na Kampuni ya simu ya Airtel ni mzuri kwani kwa sasa kila upande utapata, tofauti na miaka 19 iliyopita ambapo Serikali ilikua haipati chochote.

“Mhe. Rais Ulituagiza kuwa katika majadiliano yale tuhakikishe kwamba tunafikia makubaliano ambayo sisi kama Taifa la Tanzania Tutapata, vilevile Mwekezaji Barti Airtel naye anapata, na tukio la leo linazihirisha hilo ndiyo lililofanyika.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi