Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Amuapisha Prof. Ibrahim Kuwa Jaji Mkuu
Sep 11, 2017
Na Msemaji Mkuu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akimkabidhi hati ya kiapo Jaji Mkuu wa Mahakama Tanzania Mhe. Profesa Ibrahimu Hamisi Juma mara baada ya kumuapisha kushika wadhifa huo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Profesa Ibrahim anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mstaafu Othman Chande na kuwa jaji wa nane kushika wadhifa huo tangu tupate uhuru huku akiwa Mtanzania wa sita. Wapili kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi.

Na: Mwandishi Wetu - MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania ikiwa ni miezi nane tangu alipomteua Jaji huyo kukaimu nafasi ya Jaji Mkuu.

Sherehe za kumuapisha Jaji Profesa Ibrahim zimefanyika leo Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Jaji Kiongozi Mhe. Ferdinand Wambari, Majaji wa Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa Dini, Majaji Wastaafu na Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Serikali.

Akiongea baada ya kumuiapisha, Mhe. Rais Dkt. Magufuli amemtaka Jaji Mkuu kufanya kazi kwa weledi huku akitanguliza mbele maslahi ya Watanzania.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali na Majaji wa Mahakama Kuu Tanzania mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kumuapisha Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahimu Juma leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. (Picha na: Idara ya Habari – MAELEZO)

Pia Jaji Mkuu aliwashukuru Majaji Wakuu Wastaafu na Majaji wenzake kutokana na Rais Magufuli ameeleza kuwa haikuwa kazi rahisi kumteua Jaji Mkuu kwani nafasi hiyo inahitaji mtu makini na mwenye dhamira ya dhati ya kutenda haki na ndio maana alitumia muda wa kutosha kujiridhisha kabla ya kumteua Profesa Ibrahim kushika nafasi hiyo ya juu kabisa katika ngazi ya mahakama.

“Nilitumia muda mrefu kuteua Jaji Mkuu kwa sababu nilitaka kujiridhisha na ninaye mteua lakini pia nilitaka kuteua Jaji Mkuu atakaa muda mrefu na atakayeweza kupambana na rushwa”, alieleza Rais Dkt. Magufuli.

Katika hatua nyingine Rais amewataka Wakuu wa Mahakama, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) kukaa pamoja na kujadili namna ya kutatua changamoto za kiutendaji zinazovikabili vyombo hivyo ili haki za watu zisichelewe kutolewa pasipo sababu za msingi.

Kwa upande wake, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma alimshukuru Rais kwanza alipomteua kushika nafasi ya Kaimu Jaji Mkuu na pia baada ya kumthibitisha kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania na kuahidi kuitumikia nafasi hiyo kwa weledi na uadilifu.

ushauri na misingi thabiti waliyoiweka katika mahakama jambo lililomfanya asipate tabu katika kutekeleza majukumu yake.

Mheshimiwa Jaji Mkuu ametoa wito kwa Majaji wenzake na watumishi wa Mahakama kuhakikisha watatoa haki kwa wakati kwa kufuata utawala bora ili wananchi waendelee kuwa na Imani na mahakama.

“Kazi yetu kubwa ni kuhakikisha haki inapatikana kwa wakati kwa kufuata sharia na misingi ya utawala bora. Lazima tuendelee kupata Imani ya wananchi kwa kutenda haki”, alieleza Jaji Mkuu.

Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Hamis Juma anakuwa Jaji wa nane kushinka nafasi hiyo tangu Tanzania ipate uhuru na ni Jaji wa sita Mtanzania.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi