Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Aleta Mafuriko ya Korosho Ghalani
Nov 19, 2018
Na Msemaji Mkuu

Na: Mwandishi Wetu

Programu maalum ya HAPA NA PALE Operesheni Korosho katika Mkoa wa Mtwara imebainisha maghala yote ya Vyama vya Vikuu vya Ushirika yamesheheni korosho na sasa yanasubiri usombaji wa zao hilo kupelekwa katika maghala makuu ya bandari .

Tani zilizopo kwenye maghala mpaka sasa ni 118,193,,490 na tani zilizobaki ni 101, 807 ili kufikia tani elfu 220,000 zinazokadiriwa kupatikana kwa mwaka 2018.

Hapa na Pale imepiga hodi katika  Wilaya ya Tandahimba  yenye  jumla ya wakulima wa korosho 65,004 ambapo wamezalisha  tani  80,000 katika msimu wa kwanza wa mavuno ya awali na sasa inategemea kupeleka ghalani mavuno ya awamu ya pili takribani tani 55,000.

Hayo yamesemwa Afisa Kilimo na Umwagiliaji wa Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba Issa Naunagwa alipokutana na Hapa na Pale Operesheni  Korosho Mkoa wa Mtwara. Amesema kuwa Wilaya ya Tandahimba ina jumla ya Vyama vya Msingi 128 kati ya hivyo vilivyofanyiwa uhakiki wa kina ni Amani AMCOS, Juhudi Pemba, Mikunda,  Shumiko na Tukulu, orodha hiyo imekabidhiwa Benki ya NMB.

Aidha, Hapa na Pale ikiongea na Afisa Ushirika kwa njia ya simu Sudi Ramdhani amesema “Orodha ya wakulima imewasilishwa benki ya NMB majira ya saa 9 mchana siku ya Ijumaa na kukutwa ina kasoro kwa kuwa baadhi ya karatasi zilizohitajiwa kwa uhakiki hazikuwepo, nadhani ndio maana malipo yakashindikana kuwekwa kwenye account za wakulima”.

Hapa na Pale, ilipata fursa ya kuongea na wakulima kadhaa wa wilaya hiyo, ambao walipata fusra kutoa maoni mbalimbali kulingana na agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Joseph Magufuli kama ifuatavyo;.

Juma Mkundema ni mmiliki wa shamba la korosho lipatalo hekari  67 katika kijiji cha Kitami Wilaya ya Tandahimba, ambaye, Hapa na Pale imemkuta shambani kwake akivuna  korosho na amaeajiri zaidi ya watu 150 kwa ajili ya kuvuna kutoa mabibo kuchambua na kuziweka katika magunia.

Kwa kauli yake mwenyewe amesema “ Nashukuru kupata nafasi hii ya pekee niweze kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa kitendo cha ushujaa alichofanya.

Hakika tangu niwe na akili ya kilimo hiki sijawahi kusikia hata fununu kuwa kuna mwanasiasa, yeyote Yule acha kiongozi mabaye amefikiri kunusuru soko la korosho ambalo linasua sua kila mwaka inapofika wakati wa mavuno.

Natamani sana nikutane na Rais Magufuli niweze kumpa ushauri kuhusu zao hili alilofanya kwa kuwa mimi ni mzaliwa wa hapa na nimekulia hapa na sasa ni mkulima japo ninaishi Da-es-salaam kwa ajili ya kupanua wigo wa maisha na utafutaji wa riziki, wako wasiomtakia mema natamani sana nikutane naye.Alimalizia kwa kusisitiza Mkundema.

Kilio chetu kikubwa ni kuwa na kiwanda cha koroshoserikali na Taifa kwa ujumla linapata hasara kwa kupelka mali ghafi hii kwenye nchi nyingine na kuwatengenezea ajir awao badala ya sisi. Kama unavyooona hawa wakina mama wanahangaika hapa na pale kutafuta riziki kungekuwa na kiwanda ingesaidia sana.

Wakulima wengi wa korosho ni masikini na wenye fedha wanatumia kigezo hicho kuwarubuni na kuwafanya wawe maskini zaidi, nadhani sio sahihi kabisa sijui nifanyeje nimuone Rais niongee naye kuhusu suala la korosho wako wasiotakia mema nchi yetu wanafanya kila njia kukandamiza wakulima.

Mkundema ni mkulima mwenye shamba kubwa zaidi Tandahimba,  anategemea kuvuna zaidi ya tani 50 mwaka huu wa 2018. Hii imetokana na mvua iliyonyesha na kupukutisha maua, lakini pia amelalamikia wataalam wa kilimo ambao amesema hawana msaada. ni wazito sana kusaidia wakulima wa korosho. Mimi binafsi niliwaita hawakuja wakasema niwapigie simu na niwaeleze tatizo langu watanishauri.

Naye Mohamed Aibu ambaye ni msimamizi katika shamba la Mkundema amesema “Matatizo ya korosho ni mengi na inahitaji msaada wa ziada kutoka serikalini. Rais Magufuli amefanya jambo jema na ni mwanzo mzuri maana ametufumbua macho wakulima, maana hatukutegemea kabisa kama suala hili linaweza kufanyika maana miaka nenda miaka rudi viongozi wote wapo lakini hatukuwa na msaada”.

Mimi ombi langiu kwa Rais ni kuwa sasa wakati umefika benki ya Kilimo Tanzania kukopesha wakulima wa korosho fedha kwa ajili ya msimu wote wa kilimo. Kwa nini nasema hivyo ni kwa sanbabu wakulima wameachwa yatima na matokeo yake wanaenda kwa wanunua maua na Kangomba ambao wanawakopesha fedha wakulima na kufanya makubaliano ya kumpa kiasi fulani cha korosho.

Hivyo, unaweza kukuta mtu hana shamba la korosho lakini anakorosho nyingi tu, au unakuta hana shamba la korosho lakini kwa kuwa ana fedha anawapa wakulima na mara wanapovuna fedha yote wanayopata wanawapa wanunua maua na Kongmba kwa kuwa anadaiwa.

Sasa Rais ni lazima atengeneze mfumo mzima utakaoweza kuwainua wakulima masikini kwa kuwa kutokana na kukosa fedha za kushughulika na msimu mzima wa kilimo anazidi kuwa masikini zaidi siku hadi siku pamoja na kuwa na shamba la kulima koerosho.

Rais Magufuli asishangae, atakaposikia fedha za korosho anazowalipa wakulima wake zimeishia mikononi mwa wanunua maua au Kangomba.Pia kuna watumishi ambao sio waaminifu mfano hapa kwetu kuna wasimamizi wanakata wakulima shilingi 30 ambazo hazikuwa zinaenda AMCOS, wala Chama kikuu.

Ombi langu lingine katika Wilaya ya Tandahimba tupatiwe kiwanda cha kubangua korosho kwa kuwa wilaya yetu ni kati ya zile zinazozalisha korosho kwa wingi ili zibanguliwe hapa na kutoa fursa ya hawa wakina mama unaowaona hapa wapate ajira ya uhakika kiwandani.

Naye, Afisa Kilimo na Umwagiliaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Aford Mpanda amesema “ Halmashauri yetu ina wakulima 14,600 na itatarajia kuvuna tani 20,000.

Katika Kijiji cha Kitangari, Hapa na pale Operesheni korosho ilikutana na Katibu wa Chama cha Ushirika cha Kijiji hicho Octavian Mastaki, chenye jumla ya wakulima zaidi ya 320 kati ya hao wakulima 14,600. Ambapo wakulima 21 wamepeleka mavuno yao ya kilo 11,000   katika maghala ya Chama Kikuu cha Ushirika cha Tandahimba Newala Cooperative Union –TANECU. Orodha ambayo imewasilishwa Benki ya Micrro Finance-NMB  kwa ajili ya malipo baada ya uhakiki wa kina.

Hapa na Pale imebaini na kushuhudia wakulima wengi wapo katika chama hicho cha msingi wakichagua korosho na kuziweka katika madaraja kwa maelekezo ya maafisawa ghalani. Hakika ni mafuriko na muelekeo mzuri wa kuitikia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi