Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Ajaza Pesa Wakulima Tunduru
Nov 20, 2018
Na Msemaji Mkuu

Na Mwandishi Wetu,

Wakulima  wa Korosho wa kijiji cha  Mtonya B  katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma, wamempongeza Rais John  Magufuli kwa kuwajaza pesa ambazo tangu waanze kuuza zao hilo  hawajawahi kupewa pesa hizo kwa mkupuo kwa mauzo ya bei ya Tsh 3300 kwa kilo.

Wakizungumza Kijijini hapo leo kwa niaba ya wakulima wenzao 534 waliolipwa fedha hizo na Serikali, wakulima hao walisema, kitendo kilichofanywa na Serikali katika kusimamia bei ya zao la korosho kimedhihirisha nia ya Rais  Magufuli kusaidia wananchi wanyonge hususani wakulima.

Mmoja wa wakulima hao, Hussein Namkala alisema katika msimu huu wa kilimo amelima shamba la hekari 5 na katika mavuno yake ya awali alipata  kilo 400 ambapo katika malipo yaliyotolewa na Serikali amefanikiwa kupata Tsh Milioni 1.3.

Anaongeza kuwa Rais Magufuli ni Kiongozi wa watu ambaye anaguswa na matatizo ya Watanzania wote pasipo na ubaguzi kwani kwa wakati amekuwa akifanyia kazi kero mbalimbali za wananchi wake hususani Watanzania maskini.

“Ili kumuungaa mkono Rais Magufuli, naahidi kumtia moyo kwa kufanya kazi zaidi na kuongeza ari ya kujituma  kiasi ambacho  natarajia kuongeza hekari 3 zaidi na fedha nitakazopata zitahudumia shamba langu” anasema Namkala

Kuhusu pembejeo za kilimo katika zao la korosho, Namkala alimwomba Rais Magufuli kuwahimiza Watendaji katika Halmashauri ikiwemo Maafisa Ushirika na Kilimo kuharakisha kupatikana kwa sulphur ambayo imewayumbisha Wakulima wengi katika mwaka huu wa mavuno sana kwani wengi wao  wamelanguliwa kwa kuuziwa Tsh 50,000  na Tsh. 70,000, ambapo baadhi ya wakulima wenzao walikosa fedha hizo za kupulizia dawa.

“Tunaiomba Benki ya Kilimo Tanzania iwe mkombozi wetu wa kutukopesha fedha kwa ajili ya kuhudumia korosho na mara tunapovuna tuwalipe maana hizi Benki nyingine zinatukata riba kubwa na kipato chetu ni kidogo” alisema Namkala.

Naye Martha Chilumba  mkulima wa korosho aliyevuna kilo 303 katika shamba lake la hekari mbili amempongeza  Rais Magufuli kwa kuwajali wakulima wa wanyonge wa kijiji cha Mtonya, kwa kuwa ameonesha mfano wa Viongozi wachache wanaoguswa na maslahi ya watu wengine.

Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya Chama cha Msingi cha Mtetesi AMCOS Paulo Mlawali, Rais Magufuli amewaokoa wakulima wa kijiji hicho kutoka katika mikono ya wafanyabiashara walanguzi wa bei za korosho za wakulima na sasa matumaini ya maisha yao yamerejea baada ya kukata tamaa na kutokuwa na uhakika wa hatma ya zao la korosho.

“Wito wangu kwa Rais Magufuli  kama kuna uwezekanao akomeshe hili suala la Kangomba kwa  kuwaruhusu Benki ya Maendeo  TADB  kutukopesha fedha badala ya wakulima kulanguliwa hovyo na pia kukomesha suala la kuuibiwa kwa mizani na watendaji wasio waaminifu msimu wa korosho” alisema Mlawali.

Aidha Fauwe Mawilo ambaye ni mkulima wa hekari tano alisema katika msimu huu wa mavuno amefanikiwa kuvuna kilo 480 na kufanikiwa kupata kiasi cha Tsh Milioni 1.4, alimwomba Rais Magufuli kutoa ushauri kwa taasisi za kifedha ikiwemo mabenki kupunguza makato ya riba kwa kuwa fedha zote wanazolipwa baada ya mavuno zimekuwa zikirejeshwa kwao na wao kukosa fedha ya chakula.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi