[caption id="attachment_39231" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa meza kuu na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama na viongoz wa wafanyakazi na wa mifujo ya hifadhi ya jamii wakiwa wameshikana mikono kwa furaha huku wakiimba wimbo wa hamasa wa mshikamao wa wafanyakazi wa "Solidarity Forever" baada ya kuwasikiliza hoja zao, kuwahutubia na hatimaye kulipatia jawabu swala la vikokotoo vya wafanyakazi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Desemba 28, 2018[/caption] [caption id="attachment_39232" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa meza kuu na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama na viongozi wengine waandamizi katika picha ya pamoja na viongoz wa wafanyakazi na wa mifujo ya hifadhi ya jamii wakiwa wameshikana mikono kwa furaha huku wakiimba wimbo wa hamasa wa mshikamao wa wafanyakazi wa "Solidarity Forever" baada ya kuwasikiliza hoja zao, kuwahutubia na hatimaye kulipatia jawabu swala la vikokotoo vya wafanyakazi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Desemba 28, 2018[/caption]
Na Mwandishi Wetu - MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ameagiza wastaafu wote kwa sasa walipwe kwa kutumia Kikokotoo cha zamani cha asilimia 50 badala ya kipya ambacho kinaonekana hakieleweki miongoni mwa wastaafu na wafanyakazi.
Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo Ikulu Jijini Dar-es-salaam alipokutana na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) na Watendaji Wakuu wa Mifuko ya Jamii nchini Tanzania.
Akitoa maagizo hayo Rais Magufuli alisema: “Sasa naagiza kikokotoo cha kila mfuko kilichokuwa kinatumika kabla ya mifuko kuunganishwa yaani PSPF, PPF, GEPF, LAPF na NSSF iendelee kulipa kwa kikotoo cha asilimia 50 kulingana na taratibu walizokuwa nazo kwa muda wote hadi mwaka 2023”.
Kwa mujibu wa Rais, wanachama 50,000 wa Mfuko watakuwa wanastaafu katika kipindi cha sasa mpaka mwaka 2023.
Rais Magufuli amemuelezea mstaafu kama ni shujaa anayestahili kuoewa heshima. “Kustaafu sio dhambi na wala mtu anayestaafu kwa ajili ya kufanya kazi ni heshima maana ame-sacrifice (amejitoa sadaka) kwa ajili ya taifa hili ni shujaa hata kustaafu bila kufukuzwa ni heshima”, alisisitiza Rais.
Aidha, akionesha kukerwa na kinachoendelea katika suala zima la kikokotoo kwa wastaafu, Rais Magufuli amesema kuwa hivi sasa ni wakati wa kuwapa motisha wafanyakazi na sio kuwakatisha tamaa.
“Kitendo cha kuwaamulia wastaafu kutaka kuwalipa kidogo kidogo sio cha kiungwana, si umpe pesa yake akafie mbele badala ya kumpa asilimia 25. Kiuhalisia haingii akilini, ungefanyiwa wewe unayomfanyia mstaafu ungependa? alihoji Rais Magufuli.
Ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na Watendaji wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kusimamia na kufanya ukaguzi ili kubaini kama kuna kama kuna wastaafu hewa ili waondolewe katika orodha.
Rais Magufuli pia ameonya mifuko ya Hifadhi ya Jamii kuacha matumizi mabaya ya fedha za wanachama na badala ya fedha zitumike kulipa wastaafu mara moja. Baadhi ya matumizi mabaya ya fedha hizo kwa mujibu wa Rais ni pamoja na kutumia bilioni 1.3 kutengeneza kalenda, bilioni mbili kwa ajili ya ulinzi pekee na uwekezajikatika miradi isiyo na tija kama ule wa Dege Village.
“Hapa tunazungumzia fomula ya kikokotoo kumbe tatizo ni Mifuko wa Hifadhi ya Jamii yenyewe kwa sababu wanapeleka fedha kwenye uwekezaji ambao hazizalishi kwa sababu tu wana maslahi huko”, alieleza Rais Magufuli.
Ameitaka mifuko kuongeza idadi ya wanachama kutoka sekta mbalimbali kama kama madini na miradi mbalimbali inayoendelea nchi imeajili wafanyakazi wengi ambao wanapaswa kuwa wanachama tofauti na hali ilivyo sasa ambapo Mfuko wa NSSF UNA 400,000 tu.
Mwezi Jannuari, 2018 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilipitisha Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma Public Service Social Security Fund Act No 2 of 2018. Sheria hii iliunganishailiunganisha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PPF, PSPFna GEPF ili kuongeza ufanisi katika Hifadhi ya Jamii.
Udhaifu katika usimamaizi wa mifuko hiyo ulisababisha Serikali kuwa na deni la shilingitrilini 1.2 na wastaafu kushindwa kupata mafao yao kwa wakati. Hata hivyo hadi kufikia mwezi Machi mwaka 2017, Serikali ya Awamu ya Tano ilikuwa imemaliza kulipa deni hilo lote.
Katika mkutano huu, viongozi mbalimbali wa Serikali walihudhuria wakiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu, Mhe. Jennister Muhagama, Katibu Mkuu Kiongozi John Kijazi, baadhi ya Makatibu Wakuu, Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Dkt. Irene Isaka, Rais wa TUCTA, viongozi mbalimbali wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi na Baadhi ya Waajiri wa Sekta Binafsi.