Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Aahirisha Sherehe za Mashujaa
Jul 18, 2020
Na Msemaji Mkuu

Ikulu, Chamwino.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha sherehe za Mashujaa zilizopaswa kufanyika tarehe 25 Julai, 2020 Jijini Dodoma.


Pamoja na kuahirisha sherehe hizo, Mhe. Rais Magufuli amewataka Watanzania wote kutumia siku hiyo kuwakumbuka na kuwaombea Mashujaa wote waliojitoa kwa ajili ya nchi yetu na hata wale ambao wametoa mchango mkubwa katika ngazi mbalimbali zikiwemo mtu mmojammoja na familia.


Mhe. Rais Magufuli amewatakia heri Watanzania wote kuelekea siku hiyo na amewataka kuendelea kudumisha amani, upendo, utulivu na mshikamano.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chamwino
18 Julai, 2020

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi