[caption id="attachment_52855" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Ofisi za Ikulu Chamwino Dodoma leo Mei 30, 2020.[/caption]
Jonas Kamaleki
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango kutoa Shilingi bilioni 2 kwa ajili ya kukamilishaujenzi wa Ofisi ya Ikulu, Chamwino, Dodoma.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Ikulu, iliyofanyika leo Chamwino, Dodoma.
Akionyesha kuridhishwa na kazi inayofanywa na SUMA JKT Rais Magufuli amesema kuwa vijana 2400 wanoshiriki ujenzi huo atawafikiria ujenzi utakapokamilika.
Rais alisema kuwa kila kazi anayowapa JKT ana uhakika wanaifanya vizuri akitaja baadhi kama ujenzi wa ukuta wa Mirerani, mji wa Serikali, Dodoma na kushiriki katika misheni mbalimbali za kulinda amani ndani nan je ya nchi.
“Kweli JKT mnastahili sifa mara 100 kutokana na kazi nzuri mnayofanya, hongereni sana”, alisema Rais Magufuli.
[caption id="attachment_52857" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Marais wastaafu Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete, Ali Hassan Mwinyi na Mama Maria Nyerere ambaye ni Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa Ofisi za Ikulu ya Chamwino Dodoma leo Mei 30, 2020.[/caption]Aidha, amewapongeza watangulizi wake kwa hatua mbalimbali walizochukua kutimiza ndoto ya Baba wa Taifa ya kufanya Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi.
“Kwa kweli Nyerere aliona mbali, tangu nihamie Dodoma, nimepapenda sana, ni pazuri” alisisitiza Rais Magufuli na kuonyesha kuwa eneo la Chamwino lina mandhari ya kuvutia.
[caption id="attachment_52859" align="aligncenter" width="750"] Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa wanaoshiriki katika ujenzi wa Ofisi za Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma wakionesha umahiri wao wakati wakitumbuiza katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Ofisi za Ikulu Chamwino Dodoma leo Mei 30,2020.[/caption]Dkt. Magufuli ameongeza kuwa pamoja na ujenzi unaoendelea, tayari majengo matatu ya awali na ujenzi wa ukuta unaozunguka Ikulu vimeshakamilika. Aidha, hakuna jengo hata moja la zamani litakalobomolewa.
Kwa upande wake, Rais wa Awamu ya Pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi amemshukuru Rais Magufuli kwa uamzi wake wa kuhamishia Serikali Dodoma. Aidha, amemuelezea Rais Magufuli kuwa ni mchapakazi na mbunifu.
[caption id="attachment_52863" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin Mkapa akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Ofisi za Ikulu Chamwino Dodoma leo Mei 30,2020[/caption]Mhe. Benjamin William Mkapa, Rais wa Awamu ya Tatu amesema kuwa uamzi wa Serikali kuhamia Dodoma ni jitihada za muda mrefu na kila awamu ilifanya jitihada, Rais Magufuli amefanya mengi zaidi na sasa Serikali imehamia Dodoma.
[caption id="attachment_52864" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Ofisi za Ikulu Chamwino Dodoma leo Mei 30,2020.[/caption]Akitoa salamu kati hafla hiyo, Rais wa Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amempongeza Rais Magufuli kwa uamzi wa busara na wa hekima wa kujenga Ikulu, na kuongeza kuwa hapo ndio kilele chenyewe.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Charles Mbuge akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Ofisi za Ikulu Chamwino Dodoma, Mradi huo unatekelezwa na SUMA JKT.
Eneo la Ikulu ya Chamwino lina ukubwa wa ekari 8473 na kuonekana kuwa kubwa karibu kuliko Ikulu zote Afrika na pengine Duniani kwa ujumla.
(Picha zote na Aboubakar Kafumba)