Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiteremka ndege ya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi pamoja na Maafisa mbalimbali akitokea katika nchi ya Burundi kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan katika sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya nchi hiyo zilizofanyika tarehe 30 juni 2022.