Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar(ZSTC), Dkt. Said Seif Mzee akitowa maelezo wakati wa ziara yake kutembelea ghala la kuhifadhia karafuu katika Bandari ya Wete Pemba, zikisubiri kusafirishwa na kushoto kwa Rais ni Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Mhe.Omar Said Shaban
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuizindua meli mpya ya mizigo na abiria ya MV Ikraam 1, na kushoto kwa Rais ni Mmiliki wa Meli hiyo, Bw. Abduldhaful Ismal Mohammed, uzinduzi huo umefanyika katika Bandari ya Wete Pemba wakati wa ziara yake Kisiwani Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Nahodha wa Meli ya abiria na mizigo ya MV.Ikraam 1, wakati akitembelea meli hiyo baada ya kuizindua rasmi, hafla hiyo imefanyika katika Bandari ya Wete Pemba.