Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Dkt. Magufuli Kuanza Ziara ya Kikazi Visiwani Zanzibar.
Jan 09, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_50054" align="aligncenter" width="683"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam wakitokea mapumzikoni Chato mkoani Geita leo Alhamisi Januari 9, 2020[/caption] [caption id="attachment_50052" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dart es salaam mara baada ya
kuwasili akitokea mapumzikoni Chato mkoani Geita leo Alhamisi Januari
9, 2020[/caption]

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 09 Januari, 2020 amewasili Jijini Dar es Salaam akitokea nyumbani kwake Chato, Mkoani Geita.

Mhe. Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli kesho ataanza ziara ya kikazi Visiwani Zanzibar ambako ataweka jiwe la msingi la jengo la Idara ya Usalama wa Taifa Zanzibar.

Keshokutwa (11 Januari, 2020), Mhe. Rais Magufuli ataweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya Mwanakwerekwe iliyopo Mjini Magharibi na atafungua hoteli yenye hadhi ya nyota tano iitwayo Hotel Verde Azam Luxury Resort and Spa iliyopo Mtoni.

Mhe. Rais Magufuli atashiriki Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zitakazofanyika Jumapili tarehe 12 Januari, 2020 katika uwanja wa Amaan, Mjini Magharibi.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

09 Januari, 2020

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi