Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Picha- Operesheni Korosho ya Ukaguzi wa Maghala na Tathimini ya Malipo Kwa Wakulima wa Tunduru Mkoani Ruvuma
Nov 16, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_38307" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Japhet Justine akizungumza na wajumbe wa kamati ya Operesheni Korosho wakati alipotembelea moja ya maghala ya kuhifadhi zao la korosho katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma, jana Alhamisi (Novemba 16, 2018). Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Juma Homera.[/caption]   [caption id="attachment_38309" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma, Juma Homera akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Japhet Justine wakati alipotembelea moja ya maghala ya kuhifadhi zao la korosho katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma, jana Alhamisi (Novemba 16, 2018).[/caption] [caption id="attachment_38311" align="aligncenter" width="750"] Korosho ghafi ikwa tayari imechambuliwa na kupewa daraja la ubora katika moja ya maghala ya kuhifadhia zao hilo kwa ajili ya kusafirishwa na Kikosi maalum cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kinachoongoza operesheni maalum ya kukusanya zao la korosho katika mikoa inayozalisha zao hilo ikiwemo Lindi, Mtwara, Ruvuma na Pwani.[/caption] [caption id="attachment_38312" align="aligncenter" width="750"] Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Prof Siza Tumbo akizungumza na baadhi ya wajumbe wa kamati maalum ya kusimamia zoezi la ukusanyaji na ununuzi wa wa korosho mara baada ya kamati hiyo kufanya ziara katika moja ya maghala ya kuhifadhia korosho katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma jana Alhamisi (Novemba 16, 2018).[/caption] [caption id="attachment_38313" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuhifadhi mizigo ya DNG Paulina Mdimu akitoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Kilimo Tanzania (TADB) Japhet Justine (katikati) na baadhi ya wajumbe wengine kuhusu zoezi la uhifadhi na usafirishaji wa zao la korosho wakati wa ziara ya ujumbe wa kamati hiyo kutembelea maghala ya kuhifadhi zao la korosho Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma.[/caption] [caption id="attachment_38314" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Japhet Justine (katikati) akitazama na kuhakiki taarifa za wakulima wa zao la korosho wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Pwani kukagua taarifa na nyaraka mbalimbali za malipo ya wakulima wa zao la korosho katika Wilaya hiyo jana Alhamisi (Novemba 16, 2018).[/caption] [caption id="attachment_38315" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Japhet Justine akipiga simu ya mmoja wa wakulima wa zao la korosho katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma kwa ajili ya kujiridhisha na usahihi wa taarifa zake katika daftari la mrajis wa Chama cha Ushirika kwa ajili ya kufanyiwa malipo yake. Zoezi hilo limefanyika jana Alhamisi (Novemba 16, 2018)[/caption] [caption id="attachment_38316" align="aligncenter" width="750"] . Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Prof Siza Tumbo akizungumza na askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati wa zoezi la uhakiki wa maghala na zoezi la uhakiki wa taarifa za malipo kwa wakulima wa korosho katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma jana Alhamisi Novemba 16, 2018.[/caption] [caption id="attachment_38317" align="aligncenter" width="750"] Wabebaji na wapakiaji wa zao la korosho katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma wakiwa nje ya moja ya maghala ya kuhifadhia zao hilo wakati wa ziara ya kamati maalum ya kusimamia zoezi la ukusanyaji na malipo ya korosho kwa wakulima wa zao hilo katika Mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Pwani.[/caption] [caption id="attachment_38318" align="aligncenter" width="750"] Magunia ya shehena ya zao la korosho yakiwa yamehifadhiwa katika moja ya maghala ya kuhifadhi zao hilo katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma jana Alhamisi (Novemba 16, 2018).[/caption] [caption id="attachment_38319" align="aligncenter" width="750"] Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Prof Siza Tumbo akizungumza na wabebaji na wapakiaji wa korosho za wakulima katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma wakati wa ziara ya kamati ya kusimamia zoezi la ukusanyaji na ununuzi wa zao hilo Wilayani humo jana Alhamisi (Novemba 16, 2018).[/caption] [caption id="attachment_38320" align="aligncenter" width="750"] Akina Mama wakibangua korosho katika moja ya viwanda vya kubangulia korosho katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Pwani kama walivyokutwa na kamera yetu wakati wa ziara ya kamati maalum ya kusimamia zoezi la ukusanyaji na ununuzi wa zao la korosho kwa wakulima wa Mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Pwani.[/caption] [caption id="attachment_38321" align="aligncenter" width="750"] Akina Mama wakibangua korosho katika kiwanda cha kubangua korosho cha ETG kilichopo katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma kama walivyokutwa na kamera yetu wakati wa ziara ya kamati maalum ya kusimamia zoezi la ukusanyaji na ununuzi wa zao la korosho kwa wakulima wa Mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Pwani.[/caption] [caption id="attachment_38322" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) akitazama moja ya mifuko ya korosho iliyobanguliwa katika kiwanda cha ETG kilichopo Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma tayari kwa ajili ya mauzo wakati wa ziara ya kamati maalum ya kusimamia zoezi la ukusanyaji na ununuzi wa zao la korosho kwa wakulima wa Mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Pwani.[/caption] [caption id="attachment_38323" align="aligncenter" width="750"] Wajumbe wa Kamati maalum ya kusimamia zoezi la ukusanyaji na ununuzi wa zao la korosho kwa wakulima wa Mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Pwani wakipata maelekezo kutoka kwa mmoja wa akina mama wanaobangua korosho katika kiwanda cha ETG viwanda kilichopo katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma jana Alhamisi Novemba 16, 2018.
PICHA NA MAELEZO[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi